Loading...

Napoli yatangaza bei ya beki anayewindwa na Arsenal


Chelsea, Manchester United, Arsenal, Real Madrid na Liverpool wote wameripotiwa kuwa na nia ya kumsajili nyota wa klabu ya Napoli, Kalidou Koulibaly lakini vigogo hao wa Italia tayari wameamua kwamba watamuuza beki huyo ikiwa klabu inayomuhitaji itakuwa tayari kutoa pauni milioni 105.

Koulibaly amelitangaza jina lake na kuwa miongoni mwa mabeki wenye uwezo mkubwa kwenye Serie A, akiwa amefanikiwa kufunga magoli nane kwenye michezo 122 ya misimu minne.

Arsenal ilikuwa klabu ya mwisho kuulizia kuhusu uwezekano wa kumsajili mchezaji huyo na kwa mujibu wa taarifa ya RAI Sport, iko tayari kutoa ofa kubwa ili kumnasa raia huyo wa Senegal.

Lakini wanaweza kulazimika kukabiliana na ushindani kutoka Chelsea, Manchester United, Real Madrid na Liverpool.

Kalidou Koulibaly
Ripoti inasema kwamba Napoli haina mpango wa kumuuza beki huyo mwenye umri wa miaka 26.
Napoli yatangaza bei ya beki anayewindwa na Arsenal Napoli yatangaza bei ya beki anayewindwa na Arsenal Reviewed by Zero Degree on 5/23/2018 07:35:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.