Roma wameikataa ofa ya Real Madrid
Vigogo hao wa La Liga wametoa kipaumbele kwa usajili wa golikipa wakati ambapo Kiko Casilla anaonekana ataondoka katika klabu hiyo na Keylor Navas atafiksiha umri wa 32 msimu ujao. Wamekuwa wakihusishwa na usajili wa magolikipa kama David De Gea, Gianluigi Donnarumma na Thibaut Courtois kuelekea usajili wa kwenye majira ya joto.
Klabu hiyo inayoongozwa na zinedine Zidane, pia imeonyesha kuvutiwa na golikipa wa Roma, Alisson Becker. Ameonyesha kiwango cha kuvutia katika klabu hiyo kwwenye ligi za ndani na barani Ulaya msimu huu, na kujitangaza kuwa miongoni mwa magolikipa wenye uwezo mkubwa duniani.
Imekuwa ni mapinduzi ya ajabu kwa golikipa huyo ambaye hakucheza mchezo hata mmoja kwenye Ligi Kuu ya Italia (Serie A) msimu uliopita kabla hajafanikiwa kuliteka goli na kuwa golikipa namba moja wa klabu hiyo msimu huu.
Kiwango cha Mbrazil huyo kimeivutia klabu hiyo ya Uhispania na kwa mujibu wa ripoti mbalimbali watapeleka ofa ya karibu pauni milioni 52.25, ambayo itamfanya kuwa golikipa ghali zaidi duniani.
Pia imeripotiwa kwamba Real Madrid watampa mlinda mlango huyo mwenye umri wa miaka 25 ofa ya mkataba wa miaka mitano wenye thamani ya pauni milioni 4.35 kwa mwaka.
Lakini kwa mujibu wa ripoti ya Corrierre dello Sport, Roma wameikataa ofa hiyo kutoka Real Madrid kwa ajili ya usajili wa Alisson.
Vigogo hao wa Serie A wana hamu ya kuendelea kuwa na golikipa huyo msimu ujao na inaaminika kwamba ofa kubwa zaidi ndio pekee itakayowashawishi kumwachia Mbrazil huyo kwenye majira ya joto. Hawatakubali kiasi chochote chini ya pauni milioni 87.71 kwa ajili ya raia huyo wa Brazil.
Alisson Becker |
Hivi karibuni, Alisson aliulizwa kuhusu uwepo wa uwezekano wa yeye kwenda Read Madrid na alijibu:
“Nafurahia kusikia Real Madrid wananihitaji, ingawa mawazo yangu bado yametawaliwa na Roma hivi sasa,” aliiambia Globoesporte. “Lakini inamaanisha kwamba ninafanya jkazi yangu vizuri.”
Roma wameikataa ofa ya Real Madrid
Reviewed by Zero Degree
on
5/20/2018 08:35:00 AM
Rating: