Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 11 Mei, 2018

Malcom
Liverpool imemtaja winga wa Bordeaux, Malcom kuwa miongoni mwa wachezaji itakaowakazania  kwenye majira ya joto, huku Jurgen Klopp akilenga kuboresha safu yake ya mbele.

Manchester City inaweza kumfuatilia nyota wa Napoli, Jorginho anayekadiliwa kuwa na thamani ya pauni milioni 53 kwenye majira ya joto, Pep Guardiola akiwa amedhamiria kuongeza wachezaji wapya wenye umri mdogo katika safu ya kiungo.

Atletico Madrid wako tayari kutumia mbinu itakayoleta msisimko kumrejesha aliyekuwa straika wao, Sergio Aguero kutoka Manchester City.

Swansea wataachana na Carlos Carvalhal mwishoni mwa msimu lakini mwenyekiti wa klabu hiyo, Huw Jenkins anakusudia kupinga na hitaji la mashabiki la kumuacha aendelee.

Akiwa kwenye maandalizi ya kuteua kikosi kitakachoshiriki michuano ya Kombe la Dunia nchini Urusi, meneja wa timu ya taifa ya Uingereza, Gareth Southgate anaonekana hajamwondoa Jack Wilshere kwenye mipango yake. (Daily Mail)

Wayne Rooney anataka uthibitisho kuhusiana na hatima ya mipango ya nafasi ya meneja katika klabu ya Everton kabla hajakubaliana na uhamisho kwenda MLS. (Express)

Juventus wanataka kumsajili mshambuliaji wa klabu ya Chelsea, Alvaro Morata kwa dili la pauni milioni 15 litakalopelekea nyota huyo arejee kwenye klabu yake ya awali muda wa miaka miwili ya mkopo. (Star)

Inaonekana meneja wa Ostersunds, Graham Potter na meneja wa Bristol City, Lee Johnson wanafikiriwa na klabu ya Swansea City kama Carlos Carvalhal ataondoka mwishoni mwa msimu.

Aaron Mooy
Huddersfield wanakabiliwa na vita ya kumbakisha kiugo muhimu wa klabu yao, Aaron Mooy, huku West Ham ikiwa na hamu kubwa ya kumnasa raia huyo wa Australia.

Penekezo limeshatolewa kwa Waamuzi kutoka Ligi Kuu ya Uingereza kutoa matangazo ya moja kwa moka kuelezea maamuzi ya teknolojia ya VAR, kama wafanyavyo kwenye soka la Amerika. (Times)

Gareth Southgate anafikiria kuwaita Trent Alexander-Arnold na Jadon Sancho kwenye mipango yake ya Kombe la Dunia.

Mashujaa wa zamani wa Arsenal, Steve Bould na Jens Lehmann wanapewa ofa ya kuwa na klabu yao ya zamani kama wakufunzi.

Nyota anayewindwa na klabu ya Chelsea, Maurizio Sarri atakutana na rais wa Napoli wiki ijayo kuzungumzia kuhusu hatima yake.

Everton ina mpango wa kutumia pauni milioni 25 kumsajili beki wa klabu ya Newcastle, Jamaal Lascelles.

Nyota wa Manchester City, Yaya Toure amethibitisha kuwa anataka kuendelea kucheza soka katika Ligi Kuu ya Uingereza.

Benik Afobe anasubiria kuona kama klabu ya Wolves itamnunua baada ya kuwa na msimu mzuri katika klabu hiyo kwa mkopo, lakini mshambuliaji huyo wa Bournemouth hawazii klabu nyingine za Ligi Kuu. (Mirror)

Ryan Sessegnon 
Ryan Sessegnon anaweza kuitwa kwenye kikosi cha wachezaji 35 wa Gareth Southgate kitakachotangazwa Jumatatu. (Telegraph)

Crystal Palace imeziambia Tottenham, Chelsea, Liverpool na Man City kwamba Wilfried Zaha atagharimu pauni milioni 70.

Everton watalazimika kufikia makubaliano ya masuala ya kifedha na Wayne Rooney juu ya mwaka mmoja wa mwisho kwenye mkataba wake kabla ya uhamisho wake kwenda DC United.

Chelsea wamemwambia Mason Mount arejee kutoka Vitesse alikokuwa kwa mkopo kwa wazo la kutaka kumjuisha kwenye kikosi cha kwanza.

Cardiff wanaongoza mbio za kuwania saini chipukizi wa Newcastle, Paul Woolston baada ya kufanya vizuri kwenye muda wake wa majaribio.

Preston wanatarajia kumpa Darnell Fisher ofa ya mkataba mpya utakao kuwa na vigezo vya kumfanya akae mbali na klabu za Ligi Kuu ya Uingereza.

Fulham na Aston Villa wamejiunga na klabu ya Sheffield Wednesday kuwania saini ya nyota wa Sunderland, George Honeyman. (Sun)

Aliyekuwa meneja wa Hibernian, Mixu Paatelainen ameteuliwa kuwa meneja wa klabu ya Latvia. 

John McGinn
Steven Gerrard ana matumaini ya kutibua uhamisho wa John McGinn kutoka Hibernian kwenda Uingereza kwa kumshawishi ajiunge na Rangers. (Record)
Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 11 Mei, 2018  Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 11 Mei, 2018 Reviewed by Zero Degree on 5/11/2018 09:15:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.