Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 25 Mei, 2018

Mshambuliaji wa Liverpool, Mohamed Salah (kushoto) na Cristiano Ronaldo (kulia)
Cristiano Ronaldo amesema kuwa yeye ni 'mchezaji tofauti' sana nyota wa klabu ya Liverpool, Mohamed Salah keulekea fainali ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya Jumamosi tarehe 26 Mei, mjini Kiev.

Yaya Toure anaweza kurejea kucheza soka katika mji wa Manchester, safari hii ikiwa ni katika klabu ya Manchester United.

Xavi Hernandez amesaini mkataba wa miaka miwili klabu ya Al-Saada ya Quatar utakaomfanya aitumikie klabu hiyo hadi atakapofikia umri wa miaka 40. (ESPN)

Atletico Madrid ni miongoni mwa vilabu vinavyowania saini ya mshambuliaji wa klabu ya Chelsea, Alvaro Morata.

Leicester City na Newcastle United kwa wakati mmoja wanawania saini ya beki wa klabu ya Torino, Lorenzo De Silvestri.

Fernando Toress anaweza kuungana na Andres Iniesta aliyejiunga na Vessle Kobe chini Japan, baada ya klabu ya Sagan Tosu kutoa ofa ya kusamjili mshambuliaji huyo wa Atletico Madrid. (talkSport)
 
Meneja wa Tottenham, Maurcio Pochettino amesaini mkataba utakaomfanya aendelea kuwa mkufunzi wa Spurs hadi mwaka 2023.

Wolves inakaribia kumsajili moja kwa moja beki wa klabu ya FC Porto, Wily Boly.

Lorenzo Pellegrini
Arsenal wana hamu ya kumsajili kiungo wa klabu ya Roma, Lorenzo Pellegrini kwenye usajili wa majira ya joto.

Mshambuliaji wa klabu ya Burnley, Jonathan Walter anasema kuwa yuko sokoni baada ya kufanya mazungumzo na meneja wake, Sean Dyche.

Uhamisho wa Martin Skrtel kwenda Rangers kuungana na aliyekuwa mchezaji mwenzake katika klabu ya Liverpool, Steven Gerrard umegonga mwamba, kwa mujibu wa wakala wa mchezaji huyo.

Roy Keane bado anaweza kuamua kurejea kwenye kazi ya ukufunzi, licha ya kukiri kwamba mpira wa miguu ni 'sekta kichaa'.

Beki wa klabu ya Bournemouth, Rhoys Wiggins amelazimishwa kustaafu soka baada ya kuumia vibaya kwenye goti miezi 18 iliyopita. (Sky Sports)
 
Liverpool wana matumaini ya kukamilisha dili la uhamisho wa Nabil Fekir kwa pauni milioni 60 baada ya fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Real Madrid wikendi hii.

Aliyekuwa kiungo wa klabu ya Chelsea, Frank Lampard amefanya mazungumzo ya kuwa meneja mpya wa Derby County baada ya kujitoa kwenye mbio za kuwania kibarua cha kuinoa Ipswich. (Mirror)

Martin Dubravka anadai uhamisho wake wa pauni milioni 4 kwenda Newcastle unataegemea hatima ya Rafa Benitez.

Winga wa klabu ya Bayern Munich, Douglas Costa anayeichezea Juventus kwa mkopo
Manchester United wako tayari kulipa pauni milioni 79 kumsajili Douglas Costa, ikitokea Juventus wakishindwa kukamilisha kukamilisha chaguo la kumsajili moja kwa moja kutoka Bayern Munich.

Wolves wanajiandaa kumsajili kingo wa klabu ya Fenerbahce na Brazil, Josef de Souza.

Aliyekuwa meneja wa klabu ya West Ham, Slaven Bilic anakaribia kuwa meneja wa timu ya taifa ya China.

Manchester City watampa Phil Foden mkataba wa miaka mitano, utakaokuwa na thamani ya pauni milioni 25,000 kwa wiki atakapotimiza umri wa miaka 18 wiki ijayo. (Sun)

Meneja wa Tottenham, Mauricio Pochettino ameomba kupewa angalau pauni milioni 100 kwa ajili ya kusajili wachezji wapya kwenye majira ya joto, huku Wilfried Zaha, Anthony Martial na Ryan Sessegnon wakiwa kwenye rada za klabu hiyo.

Manchester United hawana uhakika kama wataendelea kujaribu kumsajili kiungo wa Lazio, Serjej Milinkovic-Savic baada ya klabu hiyo ya Serie A kutangaza dau la nyota huyo kuwa pauni milioni 87.5. (Daily Mail)

West Ham wameanza mchakato wa kuachana na wachezaji na benchi la ufundi chini ya uongozi wa meneja mpya, Manuel Pellegrini, ambaye ana mpango wa kufanya mabadiliko makubwa katika kikosi hicho, ikiwa ni pamoja na kusajili hadi wachezaji wapya 7 kwenye majira ya joto. (Telegraph)

Leicester ni miongoni mwa vilabu vya Ligi Kuu ya Uingereza vinavyowania saini ya nyota wa AFC Fylde, Serhat Tasdemir. (Star)

Toby Alderweireld
Manchester United wanataka kukamilisha usajili wa wachezaji wawili, Fred na Toby Alderweireld kabla Kombe la Dunia halijaanza mwezi ujao. (Times)
Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 25 Mei, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 25 Mei, 2018 Reviewed by Zero Degree on 5/25/2018 11:05:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.