Tetesi za soka barani Ulaya Jumapili Tarehe 6 Mei, 2018
Neymar Jr |
Neymar anabakia kuwa na hamu ya kuondoka Paris Saint-Germain na kutimkia Real Madrid kwa sababu anataka kucheza pamoja na mshambuliaji wa klabu hiyo, Cristiano Ronaldo. (Marca)
Klabu ya Shalke 04 ilitoa ofa kwa Southampton kumsajili Max Meyer, ambaye ataondoka kama mchezaji huru kwenye majira ya joto, lakini klabu hiyo ya Uingereza haikupoteza muda na ofa. (Bild)
Real Madrid watajaribu kumshawishi Thibaut Courtois atue Santiago Bernabeu kama watashindwa kumnasa David de Gea.
Jose Mourinho ana hamu ya kumsajili chipukizi wa klabu ya Ajax, Justin Klulvert kwenye majira ya joto. (talkSport)
Nyota wa Leicester City, Riyad Mahrez amesema kuwa aliachana na ombi lake la uhamisho lakini hatima yake katika klabu hiyo inabakia shakani.
Ufaransa imethibitisha kuwa beki wa timu ya taifa hilo na klabu ya Arsenal, Laurent Koscielny ataikosa michuano ya Kombe la Dunia.
Kiungo wa Arsenal, Santi Cazorla amerejea kwenye mazoezi ya timu hiyo baada ya miezi 18.
Arsene Wenger anaamini kuwa klabu ya Arsenal itaiubuka kueleta changamoto tena kwenye Ligi Kuu ya Uingereza baada ya yeye kuondoka. (Sky Sports)
Kiungo wa klabu ya Napoli, Sergej Milinkovic-Savic |
Wilfried Zaha yuko tayari kuondoka Crystal Palace na kusaka nafasi ya kushiriki michuano ya barani Ulaya, huku klabu kama Liverpool, Chelsea na Manchester City zikiwa na nia ya kumsajili nyota huyo.
Mohamed Salah anasema kuwa alijua kuwa anatakiwa kuondoka Chelsea miezi minne tu baada ya kujiunga na klabu hiyo, wakati Jose Mourinho alivyomtoa nje wakati wa mapumziko kwenye mchezo dhidi ya Norwich mwaka 2014.
David Moyes analenga kumfanya Jack Butland kuwa sajili yake kubwa kwenye majira ya joto, na yuko tayari kutumia pauni milioni 30 kumnasa golikipa huyo wa Stoke City.
Joe Gomez yuko hatari kuikosa michuano ya Kombe la Dunia baada ya kiungo huyo wa timu ya taifa ya Uingereza na Liverpool kupata majeraha ya kifundo cha mguu. (Sun)
Pep Guardiola amesema kuwa Fabian Delph anastahili nafasi kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza kwenye Kombe la Dunia.
Jurgen Klopp yuko tayari kuongeza nguvu kwenye kikosi cha Liverpool kwenye majira ya joto - bila kujali matokeo ya fainali ya Ligi ya Mabingwa. (Telegraph)
Chelsea wanakaribia kukamilisha usajili wa winga wa Middlesbrough, Adama Traore kwa pauni milioni 30.
Beki wa kati wa klabu ya Ajax, Matthijs de Ligt, 18 |
Manchester City wanataka kumsajili Matthijs de Ligt kwa pauni milioni 50 awe mrithi wa Vincent Kompany.
Mwenyekiti wa klabu ya Napoli, Aurelio De Laurentiis amefungua milango kwa mazungumzo ya dili la kubadilishana Antonio Conte na Maurizio Sarri kwa kumsifia meneja huyo wa Chelsea.
Manchester United inapanga dili la uhamisho wa pauni milioni 80 pamoja na Antony Martial kama sehemu ya ofa kumnasa Willian kutoka Chelsea.
Celtic imejiunga na mbio za kuwania saini ya beki wa klabu ya West Brom, Craig Dawson anayekadiriwa kuwa na thamani ya pauni milioni 15. (Mirror)
Pep Guardiola anasema kuwa Raheem Sterling anatakiwa kujifunza zaidi kwa Lionel Messi kama anataka kusonga mbele zaidi.
Steven Gerrard anataka kuomba ushauri kutoka kwa nyota wa zamani wa Liverpool na Rangers, Graeme Souness kabla ya kuanza kibarua chake.
Claude Puel ameendelea kukabiliana na shinikizo katika klabu ya Leicester baada ya mashabiki kujitokeza mbele ya bodi ya klabu hiyo wakati timu yao ilipofungwa na West Ham Jumamosi.
Alvaro Morata anasema kuwa majeraha ya mgongo na kushuka kwa kiwango chake vilipelekea mashabiki wa Chelsea kumtukana mitaani.
Mkufunzi wa timu ya taifa ya Uingereza, Gareth Southgate |
Shirikisho la Soka nchini Uingereza (FA) limemwambia Gareth Southgate kuwa anategemewa kuingoza timu ya taifa hilo walau hadi kuvuka hatua ya makundi kwenye Kombe la Dunia. (Daily Mail)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumapili Tarehe 6 Mei, 2018
Reviewed by Zero Degree
on
5/06/2018 10:40:00 AM
Rating: