Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 2 Mei, 2018

Hector Bellerin
Chelsea imejiunga na Juventus pamoja Barcelona kwenye mbio za kuwania saini ya beki wa klabu ya Arsenal, Hector Bellerin kwenye majira ya joto. (Sport)

Klabu ya Napoli ina nia ya kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid na timu ya taifa ya Ufaransa, Karim Benzema. (Don Balon)

Kiungo wa klabu ya Chelsea, N'golo Kante analengwa na Paris Saint-Germain kwenye usajili wa majira ya joto. (Le10Sport)

Liverpool itaongeza mashahara wa Mohamed Salah mara mbili ya anaolipwa sasa kumfanya aachane na mawazo juu ya uhamisho kwenda Real Madrid.

Chelsea itapeleka Tottenham kwa ajili ya kumnasa beki wa klabu hiyo, Toby Alderweireld kwenye majira ya joto. (talkSport)

Shandong Luneng ya Ligi Kuu ya China imekanusha taarifa inayodai kwamba Arsene Wenger atateuliwa kuwa mkufunzi wa klabu hiyo baada ya kuondoka Arsenal.

Meneja wa klabu ya Zenit Saint Pertersburg, Roberto Mancini amekubali kufanya mazungumzo na Italia juu kibarua cha kuinoa timu ya taifa hilo. (ESPN)

Kiungo wa St Johnstone, Blair Alston amesaini mkataba mpya wa mwaka moja katika klabu hiyo.

Kieran Tierney
Kieran Tierney anaweza kuleta mabadiliko Manchester United, kwa mujibu wa aliyekuwa mchezaji mwenzake wa zamani wa Celtic, Kris Commons.

Kylian Mbappe anasema kuwa angependelea kuona Paris Saint-Germain inamrejesha N'golo Kante nchini Ufaransa.

Klabu ya Arsenal bado haijawasiliana na Patrick Vieira kuhusiana na kuchukua nafasi ya Arsene Wenger hadi hivi sasa.

Zlatan Ibrahimovic anakiri kuwa ameikumba sana Manchester United pamoja na meneja wa klabu hiyo, Jose Mourinho. (Sky Sports)

Chelsea ni miongoni mwa klabu zenye nia kumsajili mshambuliaji wa Man United, Anthony Martial pamoja na Tottenham na Juventus.

West Ham wako tayari kulipa pauni milioni 30 kwa ajli ya kiungo wa klabu ya Chelsea, Danny Drinkwater.

Arsenal wanatafuta mkufunzi mwenye umri mdogo ambaye hataigharimu klabu awe meneja wao. (Telegraph)

Beki wa klabu ya Chelsea, David Luiz anaweza kutimkia Napoli kwenye majira ya joto ikiwa Rafa Benitez atarejea San Paolo kama meneja.

Benjamin Henrichs
Chelsea inaandaa pauni milioni 31 kwa ajili ya chipukizi wa timu ya taifa ya Ujerumani, Benjamin Henrichs, ambaye anaichezea Bayer Leverkusen.

Chelsea, Tottenham na Everton watashindania saini ya nyota wa klabu ya Spartak Moscow, Fernando.

David Moyes yuko tayari kumtema Andy Carroll kutoka kwenye kikosi cha West Ham katika vita ya kuondokana na kushuka daraja baada ya kutafutiana na nyota huyo kwenye mazoezi. (Sun)

Meneja wa Leicester, Claude Puel anaelekea kufukuzwa kazi kufuatia kipigo cha goli 5-0 dhidi ya Crystal Palace.

Arsenal wanasita kumlipa meneja wao mpya kiasi cha fedha sawa na pauni milioni 8.5 kwa mwaka, ambacho alikuwa analipwa Arsene Wenger.

West Brom wanaangalia uwezekano wa kumchukua Sam Allardyce kuwa meneja wao.

Golikipa wa Roma, Alisson amekiri kuwa amejisikia faraja kusikia kuwa Liverpool inataka kumsajili kuelekea mechi yao ya pili nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa.

Mshambuliaji wa Nice, Mario Balotelli amesistiza kuwa hatajiunga na AC Milan kwenye majira ya joto lakini amesema kuwa kuna vilabu vingi kwenye Serie A vinahitaji saini yake. (Daily Mail)

Eric Bailly
Eric Bailly ameachwa na hofu kubwa juu ya hatima yake katika klabu ya Manchester United baada ya kupotezwa na Jose Mourinho.

Uingereza ni timu ya tano kwenye orodha ya timu zinazopewa nafasi ya kutwaa Kombe la Dunia, huku nafasi ya kwanza ikikaliwa na Uhispania. (Guardian)

Luis Enrique yuko kwenye hatari ya kukosa kibarua katika klabu ya Arsenal kwa kuhitaji alipwe kiasi cha pauni milioni 15
 baada ya makato ya kodi kwa mwaka.

Max Allegri na Leonardo Jardim pia wanatazamiwa kuchukua kibaru ya kuinoa klabu ya Arsenal pia Mikel Arteta, Patrick Vieira na Julian Nagelsmann.

Meneja wa Chelsea, Antonio Conte na Maurizio Sarri wa Napoli, wanaweza kuuziana nafasi kwenye majira ya joto.

Southampton na Newcastle wanashindania saini ya kiungo wa klabu ya CSKA Moscow, Aleksandr Golovin.

Barcelona walimchunguza chipukizi wa Fulham, mwenye umri wa miaka 15, Harvey Elliot akiichezea Timu ya Taifa ya Uingereza U15 nchini Italia.

Steve Bruce anataka kumsajili straika kutoka Hull City, Abel Hernandez kama Aston Villa itapanda daraja. (Mirror)

Steven Gerrard
Steven Gerrard amekubali kuwa meneja mpya wa klabu ya Rangers baada ya kuahidiwa fedha za kutosha kuwekeza kwenye kikosi cha klabu hiyo.

West Brom wankabiliwa na kupoteza wacjezaji wengi kwenye majira ya joto, huku Jonny Evans, Nacer Chadli, Gareth Barry, Craig Dawson na James McClean wote wakitarajiwa kuondoka. (Star)

Wafanyakazi wa kitengo cha Afya cha timu ya taifa ya Uingereza wanahofia kuwa Harry Kane anaweza akawa amehatarisha nafasi ya kuitwa kwenye michuano ya Kombe la Dunia kwa kukimbilia kurejea uwanjani mapema baada ya kutoka majeruhi mwezi uliopita.

Polisi wako tayari kuwashikiria mashabiki wa Liverpool katika dimba la Stadio Olimpico hadi saa saba ya usiku kwa usalama wao kutoka kwa mashabiki wa Roma.

Uamuji juu ya kuuza Uwanja wa Wembley kwa Shahid Khan unaweza usitolewe hadi demani.

Msaidizi wa klabu ya Liverpool, Zeljko Buvac ni miongoni mwa wanaogombea nafasi ya kuwa mkufunzi wa Arsenal.

Arsenal wanataka kufanya mazungumzo na Massimiliano Allegri kuhusu nafasi ya meneja hata kama alisema anataka kubaki Juventus.

Manchester United wameanza mazungumzo ya kumuuza Matteo Darmian kwenda Juventus. (Times)

Tom Rogic
Southampton wanapitia ripoti kutoka kwa maskauti waliokuwa wanamchunguza nyota wa Celtic, Tom Rogic, huku wakiwa na nia 
pia ya kumsajili mshambuliaji wa klabu hiyo, Moussa Dembele. (Record)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 2 Mei, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 2 Mei, 2018 Reviewed by Zero Degree on 5/02/2018 10:30:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.