Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 23 Mei, 2018

Kocha msaidizi wa klabu ya Manchester City, Mikel Arteta
Mikel Arteta anatarajia kupewa mkataba mpya katika klabu ya Manchester City kufuatia kushindwa kupata nafasi ya kuinoa Arsenal.

Unai Emery hakuwa kwenye orodha fupi ya Arsenal ya wagombe wa nafasi ya meneja. (Telegraph)

Jose Mourinho aliwaambia wachezaji wa Manchester United katika wiki za mwisho wa msimu huu kwamba, wachague 'kumuunga kuno au kuondoka' Old Traford.

Javi Martinez ameiambia Liverpool kwamba, nusu ya raia wa Uhispania wanataka waifunge Real Madrid.

Brighton wanakaribia kumsajili chipukizi wa klabu ya Paris Saint-Germain, Moussa Sissako.

Leighton Baines yuko tayari kuondoka Everton na kuachana na Ligi Kuu ya Uingereza kwa ajili ya mkataba kutoka Ligi Kuu ya Marekani, MLS. (Sun)

Wachezaji wa Uingereza wanahofia uwezekano wa kubaguliwa katika Kombe la Dunia nchini Urusi. (Guardian)

Jean-Michel Seri
Arsenal wana mpango wa kumsajili Jean-Michel Seri, wakati ambapo Unai Emery anaonyesha nia ya kutaka kusajili mchezaji wake wa kwanza.

Mkurugenzi wa kandanda wa Everton, Marcel Brands atakutana na Marco Silva wiki hii kujadili mipango yao ya usajili wa wachezaji. (Daily Mail)

Rais wa Lyon, Jean-Michel Aulas ameionya Liverpool kwamba inatakiwa kuwa na fedha ya kutosha kuweza kumsajili Nabil Fekir mwaka huu. (Star)

Arsene Wenger amesema kuwa alikataa nafasi ya kuinoa klabu ya Real Madrid na timu ya taifa ya Uingereza mara kadhaa.

Arsenal na Chelsea zimejiunga na mbio za kuwania saini ya beki wa klabu ya Hamburg, Josha Vagnoman. (Express)

Chelsea wanaweza kulazimika kumlipa Antonio Conte pauni milioni 9 kama watamfukuza kazi Muitaliano huyo.

Unai Emery ataruhusiwa kuja na makocha wanne wakati atakapoanza kibaru chake rasmi katika klabu ya Arsenal. (Times)

West Ham watampa meneja mpya, Manuel Pellegrini pauni milioni 75 kwa ajili ya usajili wa wachezaji wapya.

 Alvaro Morata
AC Milan itakabiliana na Juventus kuwania saini ya mshambuliaji wa klabu ya Chelsea, Alvaro Morata kwenye majira ya joto. (Mirror)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 23 Mei, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 23 Mei, 2018 Reviewed by Zero Degree on 5/23/2018 10:50:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.