Loading...

Anayepewa nafasi kubwa kuibuka kidedea Kombe la Dunia mjini Moscow


Peru wana nafasi kubwa ya kufanikiwa kufanya vizuri kwenye Kombe la Dunia kuliko Uingereza katika kurudia kufanya tukio la kishujaa mwaka 1966, kwa mujibu wa Kampuni ya takwimu za michezo, Gracenote.


Taifa hilo kutoka Amerika ya Kusini wamepewa asilimia tano za kubeba Kombe la Dunia, ambazo ni zaidi ya kiasi kilichokokotolewa kwa Uingereza.

Peru, ambao wanashika nafasi ya 11 kwenye orodha ya viwango vya soka FIFA na wako kwenye michuano hiyo kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1982, wako kwenye Kundi C, pamoja na Ufaransa, Denmark na Australia.

Uingereza wamepewa 4%, kwa mujibu wa Gracenote
Peru wamepewa asilimia 5%, ambazo ni sawa na asilimia 1% zaidi ya Uingereza
Uingereza, ambao wanashika nafasi ya 13 kwenye orodha ya viwango vya soka FIFA, wako Kundi G, pamoja na Ubelgiji, Tunisia na Panama.

Ubelgiji na mabingwa wa Euro 2016, Ureno pia wamepewa asilimia nne za kuondoka na shangwe Julai 15, mjini Moscow.

Washindi mara tano wa michuano hiyo, Brazil ndio wanaopewa nafasi kubwa kutwaa ubingwa mwaka huu wakipewa asilimia ishirini na moja (21%), mbele ya Uhispania (asilimia kumi), Ujerumani na Argentina (wote asilimia nane).

Ufaransa (asilimia sita), Colombia na Peru (wote asilimia tano) wanamalizia orodha ya kumi bora.


Uingereza wamepewa asilimia 71% za kufuzu kwenda hatua ya mtoano - kitu ambacho walishindwa kufanya miaka minne iliyopita nchini Brazil chini ya Roy Hodgson.

Brazil ndio wanaopewa nafasi kubwa ya kutwaa Kombe la Dunia 2018, wakipewa 21%
Uhsipania wanashika nafasi ya pili, wakiwa wamepewa 10%
Hesabu hizo za kutoka Kundi G, ambalo wamo pia Ubelgiji, imetokana zimetokana hasa na utafiti juu ya Kombe la Dunia uliofanywa kampuni ya Gracenote. Wanakokotoa kwa kila alama iliyopatikana kwa kila mechi kwa kuzingatia matokeo ya kushinda/kutoa sare/kufungwa kwa kuzingatia nafasi kwenye orodha ya viwango ya FIFA.

Vijana hao wa Gareth Southgate wamepewa asilimia 41% za kushinda mchezo wao wa raundi ya 16 - ambapo watakabiliana na Poland, Senegal, Colombia au Japan kutoka Kundi H.

Kama wakivuka hatua hiyo, uwezekano wa kukutana na Ujerumani au Brazil unawasubiria na hapo ndipo alama zao zinapoanza kushuka. Uingereza wamepewa asilimia 18% za kusonga mbele zaidi kutoka hapo, huku wakipewa asilimia 8% za kuweza kushinda nusu fainali ya michuano hiyo pia.


Waingereza watakuwa na matumani ya kuunguruma na mafanikio nchini Urusi na kuthibitisha kuwa taarifa hizo zimekosewa.
Anayepewa nafasi kubwa kuibuka kidedea Kombe la Dunia mjini Moscow Anayepewa nafasi kubwa kuibuka kidedea Kombe la Dunia mjini Moscow Reviewed by Zero Degree on 6/08/2018 07:50:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.