Loading...

Hazard atoa ushauri huu kwa bodi ya Chelsea kuhusu Antonio Conte

Nyota wa klabu ya Chelsea, Eden Hazard akiwa na meneja wake, Antonio Conte
Eden Hazard ameishauri bodi ya Chelsea kufanya haraka na kuamua hatima ya Antonio Conte.


Mbelgiji huyo anataka uwazi juu ya nafasi ya meneja katika dimba la Stamford Bridge wakati akiwa na timu yake ya taifa kuelekea michuano ya Kombe la Dunia.

Hazard atakuwa mchezaji muhimu kwa Ubelgiji, wakishindania kwanza kusonga mbele kutoka Kundi G la Kombe la Dunia, ambali pia wamo uingereza.

Lakini masuala ya klabu hayako mbali sana na akili yake, na nyota huyo mwenye umri wa miaka 27 alikiri kuwa na hamu ya kutaka kujua ni nani atakuwa menja mpya wa Chelsea msimu ujao.

Kwa mujibu wa taarifa ya Mirror, Hazard alisema: "Kwa sasa nafikiria zaidi kuhusu Kombe la Dunia."

"Tulikuwa na msimu mbaya Chelsea. Tulishinda Kombe la FA mwishoni - hivyo ilikuwa ni nzuri kidogo lakini akili yangu iko kwenye Kombe la Dunia tu kwa sasa.

"Kisha naiacha bodi iiongoze Chelsea kupita njia nzuri kadri wawezavyo."

Alipoulizwa kama uamuzi juu ya Conte unaaweza kuwa na madhara juu ya hatima yake, Hazard alisema: "Ndio, ninataka kujua. Ninataka kujua, lakini kama ninavyosema kwa sasa akili yangu inafikiria Kombe la Dunia pekee.

"Kama tutakuwa na sura mpya - meneja au wachezaji - siku zote huwa ni vizuri kwa sababu ninataka wachezaji watakaoisaidia Chelsea kurejea juu msimu ujao.

"Lakini kusema kweli, dirisha la usajili bado halijashika kasi. Tutaona baadaye."
Hazard atoa ushauri huu kwa bodi ya Chelsea kuhusu Antonio Conte Hazard atoa ushauri huu kwa bodi ya Chelsea kuhusu Antonio Conte Reviewed by Zero Degree on 6/11/2018 01:26:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.