Loading...

Jeshi la Polisi kula sahani moja na wanaotapeli kwa njia ya mitandao


Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, amesema kuwa Jeshi la Polisi kushirikiana na TCRA kuna watu wanaotapeli kwa njia ya mtandao wameshawakamata na jambo hilo bado linafanyiwa kazi.

Akizungumza na Redio Times Fm, leo Juni 13, 2018 amesema kuwa jeshi lake litahakikisha linafanya juhudi wananchi hawatapeliwi.

“Utapeli ambao umekithiri ni wa kimtandao, mtu unatumiwa meseji kwamba umeshinda kiasi fulani kwa hivyo unatakiwa kutuma kiasi fulani ili upatiwe kiasi hicho, Wananchi wengi wamelizwa na utapeli huo lakini Polisi sasa hivi tunafanyia kazi,” amesema Kamanda Mambosasa.

“Sisi tuna ushirikiano wa karibu sana na TCRA na mpaka sasa kuna baadhi ya watu wanaotapeli wananchi kwa njia ya mtandao tumeshawakamata na bado tunaendelea na juhudi za kuhakikisha wananchi hawatapeliwi,” ameongeza Mambosasa.
Jeshi la Polisi kula sahani moja na wanaotapeli kwa njia ya mitandao Jeshi la Polisi kula sahani moja na wanaotapeli kwa njia ya mitandao Reviewed by Zero Degree on 6/13/2018 09:35:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.