Loading...

Manchester United yapewa ofa ya kumsajili kiungo huyu wa PSG


Jose Mourinho anatarajiwa kumuongeza Fred kwenye orodha yake ya viungo kwenye majira haya ya joto, lakini meneja huyo wa Manchester United atakuwa na nafasi ya kuongeza mwingine - ambaye amekuwa akimvutia Mreno huyo kwa muda mrefu.

Kwa mujibu wa taarifa ya Calcio Mercato, Mashetani wekundu wamepewa ofa ya nafasi ya kumsajili kiungo wa klabu ya PSG, Marco Verratti kwenye majira haya ya joto.

Marco Verratti
Inavyoonekana, Muitaliano huyo anataka kuondoka Parc des Princes na wakala wake, Mino Raiola, anatazamia kufanya jambo hilo liwezekane.

Imeripotiwa kwamba, Verratti tayari ameshakutana na meneja mpya wa PSG, Thomas Tuchel, lakini Mjerumani huyo ameripotiwa kumwambia kuwa apunguze uzito.

Sasa, hatima yake katika klabu hiyo iko shakani.
Manchester United yapewa ofa ya kumsajili kiungo huyu wa PSG Manchester United yapewa ofa ya kumsajili kiungo huyu wa PSG Reviewed by Zero Degree on 6/13/2018 10:05:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.