Loading...

Museveni: Alitaka kanisa kumfanya Mwalimu Julius Nyerere kuwa mtakatifu

Rais wa kwanza wa Tanzania Mwalimu Julius Nyerere
Rais Museveni amesisitiza kuhusu shinikizo la kulitaka kanisa kumfanya rais wa zamani wa Tanzania Julius Kabarage Nyerere kuwa mtakatifu.

Rais huyo aliwaambia wafuasi wa dini ya kikatoliki waliohudhuria sherehe za kuadhimisha siku ya Nyerere katika eneo la Namugongo kwamba kiongozi huyo alikuwa mkatoliki aliyejitolea.

'Sote tunajua vile mzee Nyerere alivyojitolea katika kanisa hili. Alikuwa kiongozi aliyejitolea na shujaa , kwa nini basi tusimwite Mtakatifu?', alisema.

Siku ya kusherehekea Julius Kambarage Nyerere ilitangazwa tarehe moja Juni 2009 wakati wa misa takatifu katika kanisa la Namugongo.

Kulingana na gazeti la The Citizen nchini Tanzania mchungaji Fr Deogratius Ssonko , anayesimamia parokia ya Namugongo alipendekeza kwamba siku hiyo itakuwa ya kuomba na kubariki.

Aliungwa mkono na Daktari Cyprian Lwanga ambaye ni Askofu wa kanisa la Archdiocese ya Kampala ambaye aliongoza misa hiyo takatifu.

Wakati wa misa hiyo ya Ijumaa rais Museveni aliahidi kuhudhuria misa kama hiyo kila mwaka kwa sababu Mwalimu Nyerere alikuwa na jukumu kubwa katika kumfanya yeye kuchukuwa uongozi wa taifa lake.

''Nitahudhuria siku hii kila mwaka. Mzee Nyerere alituunga mkono kuchukua mamlaka . Nadhani ilikuwa hatari kwa sababu watu wengine wangejitokeza ili kumpinga, na ndio maana nadhani alikuwa kingozi mzuri'', alisema.

Museveni alitaka kanisa kumfanya Nyerere kuwa mtakatifu
Rais Museveni alitoa wito kama huo alipohutubia ujumbe kutoka Kenya , Tanzania na Rwanda pamoja na mataifa mengine mwaka uliopita wakati aliposema Mwalimu nyerere ni kiongozi mkubwa zaidi kuwahi kukutana naye maishani mwake.
Museveni: Alitaka kanisa kumfanya Mwalimu Julius Nyerere kuwa mtakatifu Museveni: Alitaka kanisa kumfanya Mwalimu Julius Nyerere kuwa mtakatifu Reviewed by Zero Degree on 6/02/2018 01:05:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.