Loading...

Nyota Manchester United azungumzia kuhusu kujiunga na vigogo wa La Liga


NYOTA wa Manchester United, David De Gea amezungumzia kuhusu kuondoka katika klabu hiyo kwenda kujiunga na vigogo wa Uhispania.

Golikipa wa Manchester United, David De Gea ameonyesha kuwa hatalazimisha uhamisho wake kwenda Real Madrid kwenye majira haya ya joto.

Raia huyo wa Uhispania alidai kwamba anafurahia kuwa Manchester United.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 27 amekuwa akilengwa sana na mabingwa hao wa UEFA na alikaribia kujiunga na mabingwa hao kwenye majira ya joto 2015.

Mkataba wa sasa wa De Gea unaisha mwishoni mwa msimu ujao, ingawa United wana kipengele kinachowaruhusu kuongeza mkataba huo kwa mwaka moja zaidi.

United wamekuwa kwenye mazungumzo ya kuboresha mkataba wa De Gea baada ya Mhisapania huyo kujiendeleza hadi kufikia hatua ya kuwa miongoni mwa magolikipa bora zaidi.

David de Gea
David De Gea alisema: “Siku zote huwa niko shwari. Tarehe ya muhimu ni Juni 15.

“Kombe la Dunia ni muhimu, kwa sisi kuonyesha uwezo mkubwa, kwa timu kufanya vizuri na mambo kwenda vizuri iwezekanavyo.

“Binafsi, ninafurahia hapa nilipo, nafuraha na kwa wakati huo huo natazamia kuitumikia timu ya taifa.”
Nyota Manchester United azungumzia kuhusu kujiunga na vigogo wa La Liga Nyota Manchester United azungumzia kuhusu kujiunga na vigogo wa La Liga Reviewed by Zero Degree on 6/07/2018 07:05:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.