Loading...

Sababu za Serikali kufunga vyuo 20


Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) limefuta usajili wa vyuo 20 kwa kushindwa kufuata utaratibu wa usajili wa vyuo vya ufundi na upungufu wa rasilimali za kufundishia.

Kaimu Katibu Mtendaji wa NACTE, Dkt. Adolf Rutayuga amesema vyuo hivyo bado vina nafasi ya kuomba usajili upya endapo watarekebisha matatizo na utaratibu ukafuatwa.

“Matokeo ya uchunguzi uliofanywa kuanzia Julai 2017 mpaka Septemba 2017 ambao ulihusisha vyuo 458 ambapo 112 vya ualimu na vingine 7 vilivyokutwa haviendelei na shughuli za elimu, vyuo 426 vimekidhi vigezo lakini vyuo 32 vimekutwa na mapungufu hivyo Baraza limechukua hatua mbalimbali kwa vyuo hivyo 32,” Dkt. Rutayunga.

Pia Baraza limezuia vyuo 9 kudahili wanafunzi wapya kwa mwaka wa masomo 2018/19 na vyuo 3 vimesitishwa kutoa program zisizohidhinishwa na Baraza hilo.
Sababu za Serikali kufunga vyuo 20 Sababu za Serikali kufunga vyuo 20 Reviewed by Zero Degree on 6/08/2018 06:35:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.