Loading...

Simba SC yatinga fainali Kombe la SportPesa, kuikabili Gor Mahia ya Kenya


Mabingwa wa ligi ya Tanzania bara, Simba wametinga fainali ya michuano ya Super Cup ya kampuni ya Sportspesa baada ya kuwacharaza Kakamega Homeboyz wa Kenya kwa mikwaju 5-4 ya penalti.

Kegere amefunga mabao yote mawili ya Gor Mahia dhidi ya Singida FC
Watakutana na mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Kenya Gor Mahia ambao wameibuka washindi kwa kuwanyuka Singida FC wa Tanzania mabao 2-0, ambayo yalifungwa na Meddie Kagere.
Mashabiki wa Simba
Mechi za nusu fainali zilichezewa uwanja wa Afraha, Nakuru, ambapo Simba walifika nusu fainali baada ya kuwaondoa Kariobangi Sharks wa Kenya.

Singida FC walifika nusu fainali kwa kuwaondoa mahasimu wa jadi wa Gor Mahia AFC Leopards.

Mvua kubwa ilinyesha wakati wa mechi kati ya Gor Mahia na Singida
Kakamega Homeboyz ndio walioiwatoa mashindanoni timu kongwe nchini Tanzania, Yanga kwa kuipachika mabao 3-1 kwenye mechi ya ufunguzi.

Jumla ya dola 57,500 zitashindaniwa katika mashindano hayo na mshindi wa mashindano hayo atasafiri hadi Uingereza kutoana jasho na Everton katika uwanja wao wa Goodison Park mwezi wa saba.

Shabiki wa Kakamega Homeboyz
Bingwa mtetezi Gor Mahia ndiyo iliyocheza na Everton mwaka jana jijini Dar es Salaam ikapoteza kwa mabao 2-1, wafungaji wa Everton wakiwa ni mchezaji nyota wa zamani wa Manchester United Wayne Rooney na Kieran Dowell, naye Jacques Tuyisenge akaipa Gor Mahia bao lao moja.
Simba SC yatinga fainali Kombe la SportPesa, kuikabili Gor Mahia ya Kenya Simba SC yatinga fainali Kombe la SportPesa, kuikabili Gor Mahia ya Kenya Reviewed by Zero Degree on 6/07/2018 06:35:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.