Juventus, AC Milan kushindania saini ya nyota PSG
Rabiot hafurahii namna anavyokalia benchi PSG. Alikuwa ni mchezaji wa akiba ambaye hakutumika na PSG kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Napoli wiki hii kwa sababu alifika kwa kuchelewa kwenye mkutano ulioandaliwa na meneja wa timu hiyo, Thomas Tuchel.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 23 ameshacheza mechi 15 akiwa na PSG msimu huu, akifunga magoli mawili na kutoa 'assist' moja.
Juventus itajaribu kumshawishi Rabiot ajiunge nao kwa kumwahidi nafasi ya mara kwa mara kwenye Ligi ya Mabingwa. Ingawa, hata kama Juventus itamsajili, itakuwa ni vigumu kwa Rabiot kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza. Safi ya kiungo ya Juventus imetawaliwa na wachezaji wenye uwezo mkubwa kama Miralem Pjanic, Blaise Matuidi, Sami Khedira, Juan Cuadrado na Rodrigo Bentancur.
AC Milan watakuwa na matumaini ya kutumia uhusiano wa Rabiot na mkurugenzi wao wa kandanda Leonardo kwa faida yao.
Adrien Rabiot |
Hata hivyo, itakuwa ni vigumu sana kwa timu hizo kumsajili Rabiot kwa sababu Liverpool na Barcelona pia zimeonyesha nia ya kumsajili.
Juventus, AC Milan kushindania saini ya nyota PSG
Reviewed by Zero Degree
on
11/11/2018 03:05:00 PM
Rating: