Kocha Yanga amtimua Beno Kakolanya
Mwinyi Zahera ameweka wazi hilo jana usiku baada ya Beno kurejea kambini kwa mara ya kwanza tangu alipotoka kwenye kambi ya timu ya taifa iliyocheza na Lesotho Novemba 18, 2018.
''Nawaambia viongozi huyu mtu wamtafutie timu kabla ya dirisha la usajili kufungwa, simtaki tena ndani ya Yanga, timu zipo nyingi aende akacheze huko kwa waliokuwa wamemzuia kuja mazoezini'', alieleza Zahera.
Zahera amesisitiza kuwa anafahamu wakala wa mchezaji huyo ni miongoni mwa viongozi wa Simba hivyo hawezi kufanya naye kazi baada ya kupotea kwa muda mrefu sasa hana imani naye.
''Mtu hayupo na sisi kwa muda bila sababu maalum na tulimtafuta akawa hasemi chochote sasa kwa taarifa zilizopo ni kwamba mtu anayefanya naye kazi ni kiongozi wa Simba, na kama atarudi akakaa langoni kuachia magoli itakuwaje, yeye aende tu'', aliongeza Zahera.
Yanga ipo kambini ikijiandaa na mchezo wake wa kesho jumapili dhidi ya Ruvu Shooting utakaopigwa kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaa.

Reviewed by Zero Degree
on
12/15/2018 08:05:00 AM
Rating: