Loading...

Mashabiki Chelsea wafungiwa kwa 'kumtusi' Raheem Sterling


Klabu ya Chelsea, imewazuia mashabiki wake wanne kutoshuhudia mechi yoyote ya soka huku uchunguzi ukiendelea kuhusiana na madai ya kutoa matamshi ya ubaguzi wa rangi.

Inadaiwa kuwa walimtukana mshambuliaji wa timu ya soka ya Manchester City, Raheem Sterling.

Kisa hicho dhidi ya mwanasoka huyo mwenye umri wa miaka 24- kilitokea wakati wa mechi ambayo Man City ilicharazwa mabao 2-0 katika uwanja wa Stamford Bridge siku ya Jumamosi.


Chelsea ''inaunga mkono" uchunguzi huo wa polisi.

Taarifa kutoka katika klabu hiyo, inasema, ushahidi wa kuwepo kwa matendo na tabia ya ubaguzi wa rangi yatakuwa na matokeo ya "vikwazo vikali vya hata kutengwa au kupigwa marufuku ya maisha".

Taarifa hiyo ya timu ya soka ya Chelsea pia inaongeza kwamba, "aina yoyote ya ubaguzi na tabia ya kuudhi pia itajumuisha hukumu kama ya uhalifu".

Manchester City imeukaribisha uamuzi wa Chelsea wa kuwatimua mashabiki hao.

Taarifa ya klabu hiyo inasema: "klabu na Raheem wanashirikiana kwa karibu na mamlaka za uchunguzi zinapoendelea kuchunguza hali ilivyokuwa.

"Timu ya Manchester City na Raheem wapo tayari kufanya kazi na pande zote na taasisi zinazohusika katika malengo ya kuondosha ubaguzi mchezoni."

Watumiaji wa mitandao ya kijamii waliweka mtandaoni picha ya video ya kizaa zaa hicho, ambapo Sterling alikuwa akifokewa pale alipokwenda kuchukua mpira nyuma ya goli.

Sterling amesema "alicheka tu" aliposikia matamshi hayo, kwa sababu hakutarajia ''jingine zaidi ya hilo.''

Colin Wing, 60, amesema yeye ni mmojawapo wa mashabiki waliosimamishwa kutizama mechi, lakini ameliambia gazeti la Daily Mail kuwa, licha ya kukiri, lakini akajitetea kuwa yeye alitamka tu neno 'Manc' badala ya 'black'.

"Nimeabikia sana na tabia yangu mbaya," alisema. "naomba msamaha kwa Raheem, na nina matumaini kuwa kama mtu mwema akubali tu msamaha wangu.''

"Hata ingawa hayakuwa ubaguzi, sio vyema kabisa kwa kile nilichosema. Hata kuapa ni vibaya - lakini nilichanganyikiwa."

Shabiki mwingine, aliyejitambulisha kwa jinamoja la 'Dean', alikipigia simu kituo cha Talksport siku ya Jumatatu ili kuomba msamaha. Aliongeza kuwa: "sikusema lolote linalohusiana na ubaguzi, lakini nakubali kwamba niliapa kwa jina lake, na kumtaja kuwa ni mtu ovyo kwa Uingereza. Sijitetei."

Ujumbe wa Instagram aliotuma na Sterling mara baada ya mechi hiyo ya Jumamosi, alihoji namna vyombo vya habari vinavyowataja wachezaji weusi, jambao ambalo limesababisha mjadala mkali miongoni mwa wadau wa soka.

Shirikisho la wanakandanda mashuhuri PFA, limesema kwamba, maelezo mabaya kutoka kwa wanahabari kumhusu Sterling "inachangia zaidi matendo ya ubaguzi wa rangi", huku likiongeza kuwa mchezaji huyo wa zamani wa Liverpool, mara nyingine "ndiye anayelengwa zaidi".
Mashabiki Chelsea wafungiwa kwa 'kumtusi' Raheem Sterling Mashabiki Chelsea wafungiwa kwa 'kumtusi' Raheem Sterling Reviewed by Zero Degree on 12/11/2018 11:05:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.