Simba kushusha kiboko ya Mkude
Simba inataka kumsajili mchezaji huyo ili kuimarisha safu ya kiungo kwavile Kocha Patrick Aussems amemuelewa mavitu yake.
Ingawa Swallows wamethibitisha kupitia ukurasa wao wa Facebook jana Jumatano lakini habari kutoka ndani ya Simba zinasema kwamba ni chaguo la Aussems.
Habari zinasema kwamba Aussems amevutiwa na uchezaji wa Ndlovu ambaye anadhani ni mchezaji sahihi wa kumpa changamoto Jonas Mkude kwenye kiungo cha Simba.
Simba ingawa wana mechi ngumu dhidi ya Nkana Jumamosi jijini Kitwe, Zambia lakini vigogo wengine wanaendelea na harakati za kumaliza dili la Ndlovu kwani usajili utamalizika Jumamosi hiyohiyo wakiwa ugenini kabla dirisha halijafungwa
Simba kushusha kiboko ya Mkude
Reviewed by Zero Degree
on
12/13/2018 05:05:00 PM
Rating: