Loading...

Ajib: Tumejiandaa vizuri


Nahodha wa klabu ya Yanga, Ibrahim Ajibu amesema wanakwenda jijini Mwanza wakiwa na matumaini ya kupata pointi tatu muhimu kwenye mchezo wao wa Jumamosi dhidi ya Alliance FC.

Ajibu ameyasema hayo jioni ya leo, Februari 27, 2019 jijini Dar es salaam, wakati timu hiyo ikijiandaa kwa ajili ya safari ya kuelekea Mwanza kesho.

''Ni mchezo muhimu na mgumu, lakini maandalizi mazuri yaliyofanyika kikosini yataleta matokeo mazuri baada ya dakika 90 za mchezo'', amesema Ajibu.

Wakati huo msemaji wa Yanga Dismas Ten, ameeleza kuwa jumla ya wachezaji 20 na viongozi 8 kutoka benchi la ufundi, watasafiri kwa ndege kuelekea Mwanza, tayari kwa mchezo huo wa ligi kuu.

Mchezo huo ambao unawakutanisha wenyeji Alliance FC waliopo nafasi ya 7, dhidi ya vinara Yanga, utapigwa kwenye uwanja wa CCM Kirumba Jumamosi ya tarehe 2/3/2019 saa 10:00 jioni.
Ajib: Tumejiandaa vizuri Ajib: Tumejiandaa vizuri Reviewed by Zero Degree on 2/28/2019 07:50:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.