IGP Sirro apangua Makamanda wa Polisi Mwanza, Kinondoni
MKUU wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro amefanya mabadiliko ya makamanda wa polisi wa mkoa wa Mwanza na Kinondoni ambapo wa RPC mkoa wa Kinondoni, ACP Muliro Jumanne Muliro amekwenda kuwa RPC wa Mwanza huku ACP Jonathan Shana aliyekuwa Mwanza akihamishiwa Makao Makuu ya Polisi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Februari 5, 2019 kwa vyombo vya habari na Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, Ahmed Msangi ilieleza kuwa nafasi ya Kamanda wa kinondoni imechukuliwa na Mussa Taibu. Taarifa hiyo imeeleza kuwa mabadiliko hayo ni ya kawaida katika utendaji kazi kwa Jeshi la Polisi.
IGP Sirro apangua Makamanda wa Polisi Mwanza, Kinondoni
Reviewed by Zero Degree
on
2/05/2019 05:35:00 PM
Rating: