Kinachowaponza makocha wageni Azam hiki hapa
Cheche amesema kwa muda aliokaa ndani ya Azam FC amepata nafasi ya kuwatambua kwa ukaribu wachezaji kile wanachohitaji hali iliyompa nafasi kupata matokeo chanya kwenye mchezo wake wa kwanza.
"Unajua tatizo la wageni wengi ni kushindwa kutoa ushirikiano kwa wenyeji, wao wakija wanapenda kufanya maamuzi yao ambayo ni sahihi ila uzoefu wangu unanisaidia kupata matokeo.
"Nimekaa na wachezaji nikawajenga kisaikolojia na kuwapa maneno ya nguvu hali ambayo imewafanya wapambane na wapate matokeo chanya," amesema Cheche.
Jana Cheche aliongoza kikosi chake kikashinda mabao 3-0 mbele ya Rhino Rangers na kuifanya itinge hatua ya nane bora.
Kinachowaponza makocha wageni Azam hiki hapa
Reviewed by Zero Degree
on
2/26/2019 09:05:00 AM
Rating: