Ole Gunnar Solskjaer awaibua Ferguson, Cantona
WACHEZAJI wa Manchester United, usiku wa kuamkia jana walipata wageni wawili muhimu baada ya kufuzu kucheza robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kuifunga Paris Saint-Germain mabao 3-1.
Ugeni huo ni wa kocha wa zamani wa timu hiyo, Sir Alex Ferguson na straika wa zamani wa kikosi hicho, Eric Cantona ambao walifika kwenye vyumba vya kubadilishia nguo baada ya mchezo huo.
Kutoka kushoto ni Eric Cantona, Alex Ferguson na Ole Gunnar Solskjaer |
Wakongwe hao walionekana kuwa na furaha ambapo pamoja wakaungana na kocha wa muda wa timu hiyo kwa sasa, Ole Gunnar Solskjaer wakapiga picha pamoja.
Ferguson amekuwa akitajwa kuwa na msaada mkubwa kikosini hapo licha ya kuwa hahusiki moja kwa moja kwenye benchi la ufundi, hivyo ugeni wake kwenye vyumba ni sehemu ya kuonyesha anahusika
pia katika mafanikio ya karibuni kwa timu hiyo
Ole Gunnar Solskjaer awaibua Ferguson, Cantona
Reviewed by Zero Degree
on
3/08/2019 07:20:00 AM
Rating:
