Pigo jingine kwa Clouds Media, Mtangazaji Ephraim Kibonde afariki dunia
Kupitia ukurasa wao wa Instagram, Clouds Media wameandika:
“Tukiwa bado na majeraha mabichi ya msiba wa mMkurugenzi wetu wa Vipindi na Uzalishaji #Ruge Mutahaba, kwa masikitiko makubwa tunatangaza kifo cha Mtangazaji wetu Ephraim Kibonde kilichotokea alfajiri ya leo (Machi 7, 2019).
“Tunamtukuza Mungu kwa maisha ya Kibonde, na kumuomba yeye ampokee na kumpuzisha katika makao ya amani ya milele. Tutaendelea kuwapa taarifa zaidi kuhusiana na msiba huu. Bwana Ametoa, Bwana Ametwaa, Jina lake Lihimidiwe.

Imeelezwa kuwa, Kibonde amefariki akiwa Mwanza na alianza kusumbuliwa na presha tangu akiwa Bukoba kwenye msiba wa Ruge.
Julai 10, 2018, Kibonde alipata pigo la kuondokewa na mkewe, Sara Kibonde, ambaye alifariki dunia usiku huo wakati akipatiwa matibabu kwenye hospitali ya Hindu Mandal.
Pigo jingine kwa Clouds Media, Mtangazaji Ephraim Kibonde afariki dunia
Reviewed by Zero Degree
on
3/07/2019 08:35:00 AM
Rating: