Vikao vya kamati za Bunge kuanza leo
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa jana Jumatatu na Ofisi ya Bunge jijini Dodoma, vikao hivyo vinaanza kuanzia leo hadi Machi 30, 2019 kabla ya kuanza kwa mkutano wa Bunge la bajeti Aprili 2, 2019.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kesho Jumatano Machi 13,2019 kamati hizo za sekta zitaanza ziara za kutembelea na kukagua miradi mbalimbali na ziara za kufuatilia uwekezaji pamoja na thamani halisi ya matumizi ya fedha za umma.
Machi 22 hadi 24, 2019, Kamati za Sekta zitaanza uchambuzi wa taarifa za utekelezaji wa Bajeti kwa mwaka wa fedha 2018/2019 na makadirio ya matumizi kwa mwaka wa fedha 2019/2020 kwa mujibu wa Kanuni ya 98(2).
Vikao vya kamati za Bunge kuanza leo
Reviewed by Zero Degree
on
3/12/2019 08:05:00 AM
Rating:
