Loading...

Je, Real Madrid itamtimua kocha Zinedine Zidane hivi karibuni?


Magoli mawili ya Angel di Maria na moja la Thomas Manuer yalitosha kuipa PSG ushindi mnono wa 3-0 dhidi ya Real Madrid.

Huu ni mwendelzo wa matokeo mabaya kwa Madrid, na punde tu baada ya mchezo, mashabiki wenye hasira wenye klabu hiyo wakaanza kupiga mayowe wakitaka kocha wao Zinedine Zidane atimuliwe klabuni.

Kitu kibaya zaidi ni kuwa, licha ya PSG kupata ushindi huo mzuri, walikuwa hawana washambuliaji wao vinara wote watatu uwanjani; Neymar, Cavani na Mbappe.

Katika hesabu za nje ya uwanja, PSG ilikuwa dhaifu, lakini bado waliweza kuichakaza safu ya ulinzi ya Madrid.

Mashindano ya Klabu Bingwa Ulaya kihistoria ni ulingo wa kujidai wa Madrid, wakiongoza rekodi ya kunyakua kombe hilo mara 13, lakini kiwango walichoonesha jana usiku kinawafanya wachambuzi kujiuliza iwapo watavuka hata hatua ya makundi.

Madrid katika mchezo huo wameshindwa kupiga walau hata shuti moja lililolenga lango, na hiyo inatokea kwa mara ya kwanza toka kampuni ya Opta ilipoanza kukusanya takwimu za mechi 2003-04.

Hiki ni kipigo kikubwa zaidi kwa Madrid katika mechi ya kwanza ya Klabu Bingwa (japo pia wameshapokea kipigo kama hicho mwaka 2004 na 2005 dhidi ya Bayer Leverkusen na Lyon mtawalia.


Kwa ujumla, PSG walimiliki mpira kwa asilimia 53 didi ya 47 za Real Madrid.
Je, Zidane amefanya makosa kurudi Madrid?

Mwaka 2018, Zidane alitangaza kujiuzulu ukocha wa Real Madrid, punde tu baada ya kuingoza klabu hiyo kuchukua kombe la Klabu Bingwa Ulaya kwa misimu mitatu mfululizo.

Toka arejee klabuni mwezi Machi 2019, uwiano wake wa kupata ushindi upo chini ya asilimia 50, takwimu inayoonesha kuwa yawezekana hataweza kufanya mabadiliko yoyote ya kimsingi kuirudisha klabu hiyo kwenye kasi ya ushindi wa mfululizo.

Katika kipindi hicho ameiongoza Madrid kwenye michezo 15 ya ligi na kushinda saba, sawa na 46.7%. Santiago Solari, ambaye Zidane alichukuwa nafasi yake alishinda mechi 22 kati ya 32 kabla kutimuliwa, sawa na 68.8%.

Uwiano wa Solari haukufurahiwa na vigogo wa Madrid, na kutimuliwa baada ya miezi minne unusu kibaruani. Kwa wastani anaoendelea nao Zidane ni dhahiri kitakachomkuta kinatabirika.

Lakini hata kabla ya kuondoka mwaka 2018 mambo yalishaanza kuonekana kuwa magumu. Licha ya kushinda komble la Ulaya kwa mara ya tatu mfululizo, Madrid ilimaliza ligi ya Uhispania ikiwa nyuma kwa alama 17 mabingwa Barcelona. Hivyo ubingwa wa Ulaya, ulisitiri aibu kubwa ya nyumbani na sifa ya Zidane.

Zidane inaarifiwa kuwa alikubali kurudi Madrid kwa sababu aliambiwa asibokubali kurudi Jose Mourinho (ambaye alikuwa ameshatimuliwa na Man United) angepewa kazi hiyo, na pia aliahidiwa kuwa angekuwa na nguvu ya maamuzi kwenye usajili wa wachezaji.

Zidane ni moja ya wachezaji wazuri zaidi waliowahi kutokea duniani, lakini uwezo wake wa ukufunzi ni dhahiri si mkubwa kama wa uchezaji.

Yaaminika kuwa, mafanikio yake ya awali ndani ya Madrid yalitokana na mahusiano mazuri na maelewano baina yake na wachezaji. Lakini kuna kila dalili kuwa mahusano hayo yanavvunjika kwa kasi.

Sera yake ya uchaguzi wa mchezaji gani asajiliwe ama auzwe imeanza kulalamikiwa na baadhi ya mashabiki wa klabu hiyo.

Pia mipango yake ya kumsajili kiungo nyota wa Man Uited na Mfaransa mwenzake Paul Pogba imemwendea vibaya mpaka sasa.

Si kuwa Manchester United hawataki kumwachia Pogba, rais wa Madrid Florentino Perez ameonekana kutokutaka kumnunua kiuongo huyo.

Maoni ya wengi ndani ya Madrid ni kuwa uhisiano baina ya Zidane na Perez si mzuri.

Tayari vyombo vya habari vilivyo karibu na Perez vimeshaanza kumkosoa vikali kocha huyo.

Hali hiyo ikitokea, Zidane anapaswa kujua fika kuwa, mabadiliko makubwa huenda yakatokea.
Je, Real Madrid itamtimua kocha Zinedine Zidane hivi karibuni? Je, Real Madrid itamtimua kocha Zinedine Zidane hivi karibuni? Reviewed by Zero Degree on 9/19/2019 07:10:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.