Loading...

JPM amteua bosi Usalama wa Taifa


RAIS John Magufuli amemteua na kumwapisha Kamishna Diwani Athuman Msuya kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa.

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa, ilisema uteuzi wa Kamishna Diwani ulianza jana na alishaapishwa, Ikulu jijini Dar es Salaam. 

Kabla ya uteuzi huo, Kamishna Diwani alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).

Akizungumza baada ya kumwapisha, Rais Magufuli alimtaka kamishna huyo kuchapa kazi kwa juhudi na maarifa na kwa kuweka mbele maslahi ya taifa.

Kamishna Diwani anachukua nafasi ya Dk. Modestus Kipilimba, ambaye atapangiwa kazi nyingine.
JPM amteua bosi Usalama wa Taifa JPM amteua bosi Usalama wa Taifa Reviewed by Zero Degree on 9/13/2019 06:20:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.