Loading...

Kagere: Bocco ni pigo kubwa Simba


MSHAMBULIAJI wa Simba, Meddie Kagere, amesema kitendo cha timu yake kufunga idadi ndogo ya mabao kinatokana na kumkosa nahodha wa timu hiyo, John Bocco ambaye ni majeruhi.

John Bocco mpaka sasa hajafanikiwa kucheza mchezo wowote wa Ligi Kuu Bara kutokana na majeraha aliyoyapata wakati wa mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Azam FC.

Kwa mujibu wa gazeti la Champion, Kagere alisema kuwa, japokuwa Simba ina wachezaji wengi katika safu ya ushambuliaji, lakini kukosekana kwa nyota huyo ni pigo kwake kwani ana msaada mkubwa katika eneo la ushambuliaji.

“Simba ina wachezaji wengi sana wazuri ambao wanaweza kucheza katika eneo la ushambuliaji, lakini kukosekana kwa nahodha wetu John Bocco katika michezo iliyopita imetupunguzia vitu kama muunganiko mzuri ambao yeye akiwepo huchangia upatikanaji wa mabao mengi,” alisema.

Kagere mpaka sasa kwenye mechi mbili za ligi amefunga mabao matatu ambapo mawili aliyafunga walipoifunga JKT Tanzania mabao 3-1, kisha katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Mtibwa, alifunga moja.
Kagere: Bocco ni pigo kubwa Simba Kagere: Bocco ni pigo kubwa Simba Reviewed by Zero Degree on 9/19/2019 07:20:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.