Loading...

Samatta aandika historia mpya Genk ichapwa mabao 6-2 Ligi ya Mabingwa Ulaya



Ni historia mbili mpya Mbwana Samatta ameandika usiku uliopita. Amekuwa Mtanzania wa kwanza kucheza katika michuano ya Klabu bingwa Ulaya na pia wa kwanza kufunga goli kwenye michuano hiyo.

Hata hivyo, furaha yake ya kuweka rekodi binafsi imegubikwa na matokeo mabaya baada ya klabu yake ya KRC Genk kupokea kipigo kizito cha goli 6-2 kutoka kwa RB Salzburg.

Samatta alipachika bao lake wavuni katika dakika ya 52, lakini halikuweza kubadili mwelekeo wa mchezo sababu mpaka muda huo walikuwa nyuma kwa goli 5-1.

Awali kulikuwa na hofu juu ya afya ya Samatta na iwapo angecheza mechi hiyo baada ya kuumia goti alipokuwa akiitumikia timu ya Taifa ya Tanzania dhidi ya Burundi Hivi Karibuni.

Hata hivyo majeraha hayo madogo yalipona kabla ya mchezo wa jana usiku ambapo alicheza kwa dakika 85.

Mwiba mkali kwa safu ya ulinzi ya Genk alikuwa mshambuliaji Erling Braut HÃ¥land aliyepachika magoli matatu katika dakika ya dakika ya 2',34' na 45'.

Hii inadhihirisha kuwa, Samatta na klabu yake ya Genk itahitaji kufanya miujiza ili kuponyoka kwenye kundi hilo na kufuzu hatua ya makundi.

Historia pia haipo upande wa Genk, ikiwa hii ni mara ya tatu kwa klabu hiyo kucheza hatua ya makundi ya Champions League. Haijawahi kupata ushindi hata mmoja kwenye mechi 13 sasa.

Katika misimu hiyo ya 2002-03 na 2011-12 Genk ilimaliza mkiani kwenye makundi iliyopangiwa, n ahata sasa ipo mkiani mwa Kundi E baada ya kupokea kipigo kizito zaidi.

Genk itakutana na vinara wa kundi Napoli kutoka Italia katika mchezo ujao, huku Salzburg wakivaana na Liverpool.
Samatta aandika historia mpya Genk ichapwa mabao 6-2 Ligi ya Mabingwa Ulaya Samatta aandika historia mpya Genk ichapwa mabao 6-2 Ligi ya Mabingwa Ulaya Reviewed by Zero Degree on 9/18/2019 07:55:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.