Tetesi za soka barani Ulaya leo Ijumaa Septemba 13, 2019
Nahodha wa zamani wa klabu ya Chelsea John Terry amepigiwa upatu na mkufunzi wa zamani Roberto Di Matteo kuwa mkufunzi wa klabu hiyo katika siku za usoni. (The Athletic)
Mshambuliaji wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza Wayne Rooney anaamini Pep Guardiola angeshinda vikombe vyote iwapo angepewa ukufunzi wa timu ya Uingereza.
Manchester United wanamchunguza kiungo wa kati wa Leicester City James Maddison kuhusu uhamisho wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 msimu ujao. (Manchester Evening News)
Liverpool, Real Madrid, Barcelona na Bayern Munich zinamnyatia kiungo wa kati wa Napoli Fabian Ruiz, 23. (Calciomercato)
Mshambuliaji wa Chelsea Willian anaamini timu yake ina uwezo wa kushinda taji msimu huu licha ya mkufunzi mpya Frank Lampard kushika hatamu katika hali ngumu. (Standard)
Manchester United imeandaa kuongeza maradufu mshahara wa Victor Lindelof, 25, na kumpatia kandarasi ya mshahara wa £150,000 kwa wiki. (Sun)
Mkufunzi wa Uingereza Gareth Southgate anasema kwamba mshambuliaji wa Leicester City Jamie Vardy huenda akarudi katika kikosi cha taifa licha ya kutangaza kustaafu kutoka soka ya kimataifa mwaka uliopita . (Times)
Beki wa zamani wa klabu ya Arsenal, Per Mertesacker ametoa wito kwa kiungo wa kati Asrenal Mesut Ozil, 30, kuimarika na kutoa mchango wake kwa klabu hiyo , akisema kwamba ana kipaji ambacho hakina mchezaji mwengine wa Arsenal. (Talksport)
Mshambuliaji wa Chelsea Willian anaamini timu yake ina uwezo wa kushinda taji msimu huu licha ya mkufunzi mpya Frank Lampard kushika hatamu katika hali ngumu. (Standard)
Manchester United imeandaa kuongeza maradufu mshahara wa Victor Lindelof, 25, na kumpatia kandarasi ya mshahara wa £150,000 kwa wiki. (Sun)
Mkufunzi wa Uingereza Gareth Southgate anasema kwamba mshambuliaji wa Leicester City Jamie Vardy huenda akarudi katika kikosi cha taifa licha ya kutangaza kustaafu kutoka soka ya kimataifa mwaka uliopita . (Times)
![]() |
| Per Mertesacker |
Beki wa kulia wa Tottenham Serge Aurier, 26, amekiri kwamba anataka kuondoka katika klabu hiyo msimu huu. (Football.London)
Winga wa Everton Yannick Bolasie, 30, ambaye kwa sasa yuko katika klabu ya Sporting Lisbon, anatumai kwamba kandarasi yake itafanywa kuwa ya kudumu msimu ujao. (Record)
Winga wa Everton Yannick Bolasie, 30, ambaye kwa sasa yuko katika klabu ya Sporting Lisbon, anatumai kwamba kandarasi yake itafanywa kuwa ya kudumu msimu ujao. (Record)
Chanzo: BBC
Tetesi za soka barani Ulaya leo Ijumaa Septemba 13, 2019
Reviewed by Zero Degree
on
9/13/2019 08:20:00 AM
Rating:
Reviewed by Zero Degree
on
9/13/2019 08:20:00 AM
Rating: