Tetesi za soka barani Ulaya leo Jumanne Septemba 17, 2019
Liverpool walipanga kumsajili mlinzi wa kati wa Napoli na Senegal Kalidou Koulibaly iwapo mipango yao ya kumsajili beki kisiki wa Uholanzi Virgil van Dijk, ingegonga mwamba mwezi Januari 2018. (Goal)
Klabu ya Celtic ya Uskochi inaweza kujaribu kumsajili kiungo wa klabu ya Tottenham na Timu ya taifa ya Kenya Victor Wanyama, 28, mwezi Januari, kwa mujibu wa kocha wa klabu hiyo Neil Lennon. Wanyama aliwika na Celtic kabla ya kutimkia England, na sasa kocha wa Tottenham ameshaeleza kuwa hana haja naye. (Team Talk)
Winga wa Chelsea na Brazil Willian anataka kusalia kwenye uga wa Stamford Bridge, lakini klabu hiyo hata hivyo bado haijampatia nyota huyo mwenye miaka 32 mkataba mpya. (Express)
Beki wa Ajax na Uholanzi Joel Veltman, 27, amebainisha kuwa alitaka kujiunga na klabu ya West Ham United ya England katika dirisha la usajili lililopita lakini mabingwa hao wa Uholanzi hawakumruhusu kuindoka. (NOS)
Everton, Southampton, Bournemouth, Sheffield United, Bristol City, Barnsley na Sunderland wote wanamfuatilia kwa makini winga kinda wa klabu ya Motherwell ya Uskochi James Scott, 19.
Meneja wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer ataendelea na mipango ya kusajili wachezaji kutoka Uingereza msimu ujao wa dirisha la usajili la majira ya joto.
Bournemouth pia wanaweza kumpoteza mshambuliaji wao Callum Wilson, 27, anayenyemelewa na Manchester United.
James Maddison, 22 |
Wachezaji ambao wapo kwenye rada ya Solskjaer ni mshambuliaji kinda wa England na klabu ya Borussia Dortmund Sancho, 19, na kiungo wa Leicester City na England James Maddison, 22. (ESPN)
Miamba ya soka ya Italia, vilabu vya AC Milan, Inter Milan, Juventus na Borussia Dortmund zote zipo kwenye mipango ya kutaka kumsajili kiungo wa Manchester United Nemanja Matic, 31, pale mkataba wa mchezaji huyo wa kimataiifa wa Serbia utakapofikia tamati mwishoni mwa msimu huu. (Calcio Mercato)
Bournemouth wanajiandaa kumpatia Ryan Fraser, 25, mkataba mpya wenye thamani ya pauni 100,000 kwa wiki. Tayari vilabu vya Arsenal, Everton, Chelsea na Wolves vyote vinamnyemelea winga wa Uskochi. (90min.com)
Beki wa klabu ya Watford na Ubelgiji Christian Kabasele, 28, amebainisha kuwa anakaribia kusaini mkatabampa na klabu yake. (Sport Witness)
Chanzo: BBC
Tetesi za soka barani Ulaya leo Jumanne Septemba 17, 2019
Reviewed by Zero Degree
on
9/17/2019 07:20:00 AM
Rating: