UEFA: Dortmund, Barcelona zatoka suluhu, Chelsea, Liverpool, KRC Genk hoi
Mlinda lango wa Barca Marc Andre ter Stegen aliuokoa mkwaju wa penalti uliopigwa na nahodha wa Dortmund Marco Reus kunako kipindi cha pili.
Viongozi wa Ligi Kuu ya Ujerumani RB Leipzig nao wamefanikiwa kuchukua alama zote tatu baada ya kuwalaza miamba wa Ureno Benfica mabao mawili kwa moja.
Mshambuliaji Timo Werner ndiye aliyewafungia Leipzig mabao yote mawili na kuhakikisha kwamba mkufunzi Julian Nagelsmann anapata ushindi wake wa kwanza katika Champions League baada ya mechi saba katika taaluma yake ya ukocha.
Kwa upande mwingine Chelsea ilishuka dimbani jana dhidi ya Valencia katika mchezo wao wa kwanza uliochezewa Stamfod Bridge, ambao ulimalizika kwa wababe hao wa darajani kuambulia kichapo cha bao 1-0 licha ya kuonyesha juhudi kubwa za kutafuta ushindi.
KRC Genk ilikubali kichapo cha mabao 6-2 dhidi ya Red Bull Salzburg |
Mchezo mwingine ulikua kati ya Redbull Salzburg na KRC Genk, anayochezea Mtanzania Mbwana Samatta ulimalizika kwa Genk kukubali kichapo cha mabao 6-2.
Ukiachana na michezo hiyo, jana bingwa mtetezi wa michuano hiyo Liverpool alianza kwa kichapo cha mabao 2-0 dhidi ya Napoli.
Leo hii mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich watateremka dimbani kucheza na Red Star Belgrade.
Matokeo ya mechi nyingine zilizochezwa jana ni kama ifuatavyo:
- Inter Milan 1-1 Slavia Prague
- Lyon 1-1 Zenit
- Ajax 3-0 Lile
- Benfica 1-2 B Leipzig
UEFA: Dortmund, Barcelona zatoka suluhu, Chelsea, Liverpool, KRC Genk hoi
Reviewed by Zero Degree
on
9/18/2019 07:35:00 AM
Rating: