Vigogo Chadema wana kesi ya kujibu
Mbali ya Mbowe, washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Katibu Mkuu Taifa, Dk Vincent Mashinji, Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa, Naibu Katibu Mkuu Taifa, Zanzibar, Salum Mwalimu, Mbunge wa Kibamba, John Mnyika, Katibu Mkuu Taifa, Vicent Mashinji, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee, Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, Mbunge wa Tarime Mjini, Ester Matiko na Mbunge wa Bunda, Ester Bulaya.
Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba alitoa uamuzi huo jana baada ya upande wa mashitaka kufunga ushahidi wao. Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi alidai mashahidi nane wanatosha kuthibitisha kesi yenye mashitaka 13 yanayowakabili washitakiwa hao hivyo, wanafunga ushahidi dhidi ya kesi yao.
Baada ya kueleza hayo, Hakimu Simba alisema washitakiwa wote wana kesi ya kujibu kama wanavyokabiliwa na mashitaka katika mahakama hiyo. Alisema kwa mujibu wa kifungu cha 231 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA), washitakiwa watatakiwa kujitetea kwa kiapo, bila kiapo au kwa kukaa kimya. Aliwataka washitakiwa hao kuwasiliana na mawakili wao kuhusu kujitetea.

Hakimu Simba aliahirisha kesi hiyo hadi Septemba 17, 18 na 19, mwaka huu itakapokuja kwa ajili ya kujitetea. Washitakiwa hao wanakabiliwa na mashitaka 13 likiwemo la kula njama; ambao wote wanadaiwa kuwa Februari Mosi na 16, mwaka jana, Dar es Salaam walikuĺa njama ya kutenda kosa la kufanya mkusanyiko usio halali na kukiuka tamko la kutawanyika.
Wanadaiwa Februari 16, mwaka jana katika viwanja vya Buibui na Mwananyamala Kinondoni wakiwa walikusanyika na azma ya pamoja, waliitekeleza kwa kufanya mkusanyiko usio halali na kusababisha watu waogope kuwa watakwenda kupelekea uvunjïfu wa amani.
Pia wanadaiwa kuwa Februari 16, mwaka huu katika barabara ya Kawawa Kinondoni Mkwajuni washitakiwa hao wakiwa na wenzao 12 ambao hawapo mahakamani walikiuka tamko la kuwataka kutawanyika la Ofisa wa Polisi SSP, Gerald Ngiichi kwa kugoma kutawanyika na kupelekea uvunjifu wa amani.

Inadaiwa kugoma huko kulipeĺekea hofu na hatimaye kusababisha kifo cha Akwilina Akwiline na majeruhi kwa askari wawili ambao ni H.7856 PC Fikiri na E.6976 CPL Rahim Msangi.
Chanzo: Habari Leo
Vigogo Chadema wana kesi ya kujibu
Reviewed by Zero Degree
on
9/13/2019 07:15:00 AM
Rating: