JPM akamilisha uteuzi wa Baraza la Mawaziri
Rais Magufuli amekamilisha uteuzi wa Baraza la Mawaziri. Hii leo Baraza limetangwaza ambapo jumla ya Mawaziri 21, na kufanya idadi yao kuwa 23.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi, Mhandisi John William Kijazi amesema pia Rais Magufuli amefanya uteuzi wa Naibu Mawaziri 23 na Makatibu Wakuu wa wizara mbalimbali.
Pia amewateua wabunge wawili ambao pia amewapa nafasi ya uwaziri.
Katika orodha iliyotangazwa leo baadhi ya mawaziri wamerejea katika nafasi zao, wengine wakipanda kutoka manaibu waziri na kuwa mawaziri kamili.
Kuna sura mpya zilizojitokeza kwenye baraza hilo, halikadhalika baadhi ya mawaziri katika baraza lililopita wakihamishiwa katika wizara nyingine.
Mawaziri waliosalia katika nafasi zao ni Profesa Joyce Ndalichako (Wizara ya Elimu), Dotto Biteko (Wizara ya Madini), Jenista Mhagama (Ofisi ya Waziri Mkuu), Selemani Jaffo (Tamisemi) na George Simbachawene (Mambo ya Ndani).
Wengine waliorejea kwenye nafasi zao ni Mwigulu Nchemba (Sheria), William Lukuvi (Ardhi), George Mkuchika (Utumishi), Medard Kalimani (Nishati).
Baadhi ya mawaziri wa awamu iliyopita wamerejea lakini wamehamishwa wizara; nao ni Ummy Mwalimu ambaye sasa ni Waziri wa Muungano na Mazingira kutoka Wizara ya Afya na Innocent Bashungwa ambaye sasa ameteuliwa kuongoza wizara ya Habari na Michezo akitoka Wizara ya Viwanda.
Waliokuwa Manaibu Mawaziri na sasa wamepanda na kuwa Mawaziri kamili ni Dkt Damas Ndumbaro (Maliasili na Utalii), Dkt Faustine Ndungulile anayesimamia wizara mpya (Mawasiliano na Teknolojia) , Elias John Kwandikwa ( Ulinzi) Mashimba Ndaki (Mifugo na Uvuvi) na Juma Aweso (Maji).
Sura mpya zilizopenya ni Prof Kitila Mkumbo (Ofisi ya Rais, Uwekezaji), Prof Adolph Mkenda (Kilimo), Geofrey Mwambe (Viwanda na Biashara)
Sura nyingine mpya ni waliokuwa makatibu wakuu ambao sasa wameteuliwa kuwa mawaziri; nao ni Dkt Leonard Chamuliho (Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi) na Doroth Gwajima (Afya).
Watuele hao wanatarajiwa kuungana na Profesa Palamagamba Kabudi (Wizara ya Mambo ya Nje) na Dkt Philip Mpango (Wizara ya Fedha na mipango) ambao tayari wameshaapishwa.
ORODHA KAMILIA YA BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI HII HAPA CHINI:
- Wizara ya Maji -Aliyeteuliwa Jumaa Aweso
- Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo - Aliyeteuliwa Innocent Bashungwa
- Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Vijana na Wenye Ulemavu - Aliyeteuliwa Jenister Mhagama.
- Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto - Aliyeteuliwa Doroth Gwajima (Mbunge mpya alikuwa Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI-Afya)
- Wizara ya ofisi ya rais uwekezaji - Prof. Mkumbo Kitila
- Wizara ya Katiba na Sheria - Aliyeteuliwa Mwigulu Nchemba.
- Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia - Aliyeteuliwa Prof Joyce Ndalichako.
- Wizara ya Mifugo na Uvuvi - Aliyeteuliwa Mashimba Mashauri Ndaki.
- Wizara ya Maliasili na Utalii - Aliyeteuliwa Dkt Ndumbalo Damas.
- Wizara ya Ofisi ya Rais - TAMISEMI Selemani Jaffo
- Wizara ya Madini - Aliyeteuliwa Dotto Biteko
- Wizara ya Nishati - Aliyeteuliwa Dkt Medard Kalemani.
- Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi - Aliyeteuliwa (mbunge mpya), Mhandisi Dkt Leonard Chamuliho (alikuwa Katibu Mkuu Uchukuzi).
- Wizara ya Kilimo - Aliyeteuliwa Prof.Adolph Mkenda.
- Wizara ya Viwanda na Biashara - Aliyeteuliwa Mwambe Geofrey Idelphonce.
- Wizara ya Mambo Ya Ndani - Aliteuliwa George Simbachawene.
- Wizara ya Muungano na Mazingira - Ummy Mwalimu.
- Wizara ya (Wizara mpya) ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari- Aliyeteuliwa Dkt Faustine Ndugulile.
- Wizara ya Fedha - Aliyeteuliwa Dkt Philip Mpango.
- Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki - Aliyeteuliwa Prof Palamagamba Kabudi.
- Wizara ya Ardhi- Aliyeteuliwa William Lukuvi
- Wizara ya Ulinzi na JKT- Aliyeteuliwa Elias John Kuandikwa.
- Wizara ya Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora - Aliyeteuliwa Capt Mstaafu George Mkuchika.
Wateule hao wanatarajiwa kuapishwa wiki ijayo.
JPM akamilisha uteuzi wa Baraza la Mawaziri
Reviewed by Zero Degree
on
12/05/2020 06:50:00 PM
Rating: