Madiwani wapiga kura ya kutokuwa na imani na Mike Sonko
Madiwani 88 kati ya 122 wa kaunti ya Nairobi wamepiga kura ya kutokuwa na imani na Gavana wa Nairobi, Mike Sonko hii ni idadi ambayo imepitisha kiwango cha theluthi tatu kumuondoa gavana aliyemadarakani.
Kwa mujibu wa taarifa, kitakacho fuata sasa ni wasilisho la matokeo hayo mbele ya bunge la Seneti ambapo hatma ya gavana wa Nairobin imo mikononi mwao.
Awali, gavana huyo alikuwa ametuma ombi katika mahakama kuu kusitisha hatua ya kuondolewa kwake akisema kwamba ni kinyume cha sheria na kinyume na katiba vilevile.
Kwa gavana ambaye kipindi fulani alikuwa mwenye nguvu na utawala wa aina yake, ikiwa bunge la seneti litadumisha matokeo ya kura ya kutokuwa na imani naye yaliyowasilishwa na bunge la kaunti, kitakachofuata itakuwa ni kuandaliwa kwa uchaguzi mpya katika kaunti hiyo kumchagua gavana na naibu wake na kutamatisha utawala wa gavana huyo aliyekuwa na madoido ya kipekee.
Na pia ikumbukwe, hadi anapigiwa kura ya kutokuwa na imani naye, Sonko alikuwa hana naibu gavana.

Je ni mwisho wa ugavana wake?
Kwa gavana ambaye kipindi fulani alikuwa mwenye nguvu na utawala wa aina yake, ikiwa bunge la seneti litadumisha matokeo ya kura ya kutokuwa na imani naye yaliyowasilishwa na bunge la kaunti, kitakachofuata itakuwa ni kuandaliwa kwa uchaguzi mpya katika kaunti hiyo kumchagua gavana na naibu wake na kutamatisha utawala wa gavana huyo aliyekuwa na madoido ya kipekee.
Na pia ikumbukwe, hadi anapigiwa kura ya kutokuwa na imani naye, Sonko alikuwa hana naibu gavana.
Madiwani wapiga kura ya kutokuwa na imani na Mike Sonko
Reviewed by Zero Degree
on
12/04/2020 07:10:00 AM
Rating: