Majina ya waliopanguliwa Dawasa haya hapa
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira (Dawasa) imefanya mabadiliko ya watendaji katika nafasi mbalimbali pamoja na kuongeza mikoa saba ya huduma.
Mabadiliko hayo yametangazwa leo Alhamisi Desemba 24, 2020 na ofisa mtendaji mkuu wa mamlaka hiyo, Cyprian Luhemeja ikiwa na utekelezaji wa agizo la waziri wa maji, Jumaa Aweso, alilolitoa jana akitaka yafanyike mabadiliko ya watendaji ili kuboresha huduma za upatikanaji wa maji.
Waliotakiwa kufanyiwa mabadiliko hayo ni watendaji wa Tabata, Temeke, Tegeta, Ilala, Magomeni, Kigamboni, Mkuranga, Kisarawe, Mbezi, Bagamoyo, Chalinze, Kibaha, Ubungo, Kinondoni na Ukonga.
Luhemeja amewataja mameneja waliobadilishwa na majina ya vituo vyao vipya; Pascal Fumbuka (Chalinze), Alpha Ambokile (Kibaha), Judith Singinika (Kawe), Gilbert Masawe (Ubungo), Alex Ngwandu(Kisarawe).
Christian Kaoneka (Bagamoyo), Erasto Emmanuel (Kinondoni), Victoria Masele (Tegeta), Boniface Philemon (Tabata), Jullieth John (Magomeni), Tumain Mhondwa (Kigamboni) na Damson Mponjoli(Ukonga), Abraham Mwanyamaki (Mkuranga), Crossman Makele (Temeke) na Honest Makoi(Ilala).

Kuhusu mikoa ya kihuduma saba iliyoongezwa ili kuwafikia zaidi wananchi Luhemeja ameitaja kuwa ni Kibamba, Makongo, Mabwepande, Kinyerezi, Mbagala, Mivumoni na Mapinga.
“Mpaka sasa tayari uongozi umefanya uteuzi wa mameneja wapya ambao ni Redemta James (Mbagala), Deosdedith Kimaro (Mivumoni), Edson Robert (Makongo), Haruna Taratibu ( Mabwepande), Mkashida Kavishe (Mapinga), Burton Mwalupaso(Kinyerezi) na Elizabeth Sankere(Kibamba).
Ofisa huyo pia amefanya mabadiliko katika menejimenti ikiwemo nafasi ya meneja rasilimali watu ikichukuliwa Bernadetha Mwabusila na Stella Fumbuka katika nafasi ya meneja utawala.
Ofisa huyo pia amefanya mabadiliko katika menejimenti ikiwemo nafasi ya meneja rasilimali watu ikichukuliwa Bernadetha Mwabusila na Stella Fumbuka katika nafasi ya meneja utawala.
Majina ya waliopanguliwa Dawasa haya hapa
Reviewed by Zero Degree
on
12/24/2020 11:44:00 AM
Rating: