Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya leo Jumatatu Disemba 21, 2020



Marseille ingependelea kumsajili mshambuliaji wa Chelsea na Ufaransa Olivier Giroud, 34. (le10sport )

Liverpool inafikiria kumuuza mshambuliaji wa Misri asiye na raha Mohamed Salah, 28, kulingana na mshambuliaji wa zamani wa Misri Mohamed Aboutrika. (Bein Sports)

Real Madrid ina matumaini ya kumsajili mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, 22, kutoka klabu ya Paris St-Germain msimu ujao. (90 Min)

Mwenyekiti wa klabu ya Bayern Munich Karl-Heinz Rummenigge amekubali kwamba beki David Alaba, 28, anatarajiwa kuondoka katika klabu hiyo ya Ujerumani.

Kandarasi ya raia huyo wa Austria inakamilika tarehe 30 mwezi Juni 2021 , na mchezaji huyo anaweza kuanza mazungumzo na klabu yoyote anayotoka kuanzia mwezi tarehe mosi mwezi Januari, huku klabu ya Real Madrid ikitarajiwa kumnyakua. (Marca)

Kiungo wa kati wa zamnai Roy Keane anaamini Manchester United inaweza kuikabili Liverpool kuwania taji la ligi kuu na huenda wakaipatia Liverpool changamoto mdsimu huu. (Sky Sports)

Slaven Bilic alijua kwamba atafutwa kazi na West Brom aliporudi katika ziara ya Manchester City wiki iliopita. (Telegraph)

Mkufunzi wa Juventus Andrea Pirlo amepinga uwezekano wa uhamisho wa nyota wa Argentina Paulo Dybala, 27. (Mail)



Manchester United ina hamu ya kumsajili mchezaji anayelengwa na Arsenal pamoja na liverpool Yves Bissouma, mchezaji wa klabu ya Brighton na raia wa Malian mwenye umri wa miaka 24 ambaye ameonesha mchezo mzuri msimu huu. 

Manchester City iko tayari kufikiria ofay a kumsajili bei wa Ukraine Oleksandr Zinchenko, 24, katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari. (Express)

Beki wa Ujerumani Antonio Rudiger, 27, amekiri hafurahii hali yake katika klabu ya Chelsea, lakini anasisitiza kwamba hatatafuta uhamisho mwezi Januari. (ZDF)

Winga wa Japan Takefusa Kubo, 19, huenda akakatiza uhamisho wake wa mkopo katika klabu ya mwezi Januari baada ya kukosana na kocha Unai Emery. (As)

Chanzo: BBC
Tetesi za soka barani Ulaya leo Jumatatu Disemba 21, 2020 Tetesi za soka barani Ulaya leo Jumatatu Disemba 21, 2020 Reviewed by Zero Degree on 12/21/2020 09:25:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.