Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya leo Jumamosi Disemba 26, 2020



Mkufunzi wa zamani wa Tottenham Hotspur Mauricio Pochettino anataka kumleta mshambuliaji wa Barcelona na Argentina Lionel Messi, 33, Paris St-Germain. Pochettino anapigiwa upatu kuchukuwa wadhifa wa ukufunzi katika klabu hiyo ya bingwa ya Ufaransa baada ya Thomas Tuchel kufutwa Alhamisi. (Le Parisien)
Kiungo wa kati wa England Dele Alli, 24, huenda akaondoka Spurs wakati Pochettino atakapojiunga na klabu ya Ligue 1. (Sun)

Juventus na AC Milan wameingi akatika kinyang'anyiro cha kumsaka mshabuliaji wa Celtic Mfaransa Odsonne Edouard, 22. (Calciomercato)

Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp amemwambia mshambuliaji wa Misri Mohamed Salah sababu pekee ya kuondoka Ligi ya Primia ni hali ya hewa lakini amekubali kuwa klabu hiyo haiwezi kumlazimisha mchezaji kusalia nao bila hiari yake. (Guardian)

Jurgen Klopp amwambia Mohamed Salah sababu pekee ya kuondoka Ligi ya Primia ni hali ya hewa

Kiongo wa kati wa Arsenal Mjerumani Mesut Ozil, 32, amefany amazungumzo ya siri na Fenerbahce katika juhudi za kutaka kuondoka Gunners. (Bild )

Ozil ana uhakika hataregeshwa katika kikosi cha kwanza cha Arsenal nusu ya pili ya msimu na hakuna uwezekano wa kuhamia Marekani. (INews)
Tetesi za soka barani Ulaya leo Jumamosi Disemba 26, 2020 Tetesi za soka barani Ulaya leo Jumamosi Disemba 26, 2020 Reviewed by Zero Degree on 12/26/2020 03:02:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.