Loading...

Simba SC yaibuka kidedea dhidi ya Ruvu Shooting, CCM Kirumba leo



KIKOSI cha Simba leo Novemba 19 kimeibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Ruvu Shooting kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa CCM Kirumba.
Kwenye mchezo leo, Simba ilikuwa bora kipindi cha kwanza na iliweza kufunga mabao yote matatu kupitia kwa Meddie Kagere dakika ya 17 na 36 pamoja na Kibu Dennis ambaye alipachika bao dk 44.

Kipindi cha pili kilitawaliwa na Ruvu Shooting ambao waliweza kucheza kwa utulivu mkubwa na walipata bao la kufutia machozi kupitia kwa Elias Maguli aliyepachika bao dk 70.

Nyoni hakuwa na bahati leo kwa kuwa mikono mia ya Mohamed Makaka iliweza kuzuia penalti aliyopiga dakika ya 71 baada ya Kibu kuchezewa faulo ndani ya 18.

Mpaka dakika 90 zinakamilika Simba imeweza kuondoka na pointi tatu na ushindi wa mabao matatu ukiwa ni ushindi mkubwa kwa Simba msimu huu kwa kuwa kwenye mechi za awali ilikuwa inashinda bao mojamoja.

Inafikisha pointi 14 inabaki nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi na kinara ni Yanga mwenye pointi 15.

Pia rekodi ya bila kufungwa ya Manula imetiwa dosari na Maguli ambaye amemfunga Manula katika Uwanja wa CCM Kirumba.
Simba SC yaibuka kidedea dhidi ya Ruvu Shooting, CCM Kirumba leo Simba SC yaibuka kidedea dhidi ya Ruvu Shooting, CCM Kirumba leo Reviewed by Zero Degree on 11/19/2021 06:50:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.