Loading...

Utatuzi mgogoro wa Sudan bado haujapatikana

Picha na ABNA

Jeshi la sudan bado linafanya mashauriano na Waziri mkuu aliyetimuliwa katika mapinduzi ya wiki iliyopita dhidi ya makubaliano yanayoweza kumrejesha Waziri mkuu , vyanzo vya habari vya karibu vimesema Jumatano.

Vyanzo hivyo vilikanusha ripoti kuwa Abdalah Hamdock amekubali kurejea kuongoza serikali.

Hamdock amekuwa katika kifungo cha nyumbani tangu serikali yake ilipotimuliwa na jenerakli mkuu wa jeshi Abdel Fattah al Burhan kwenye mapinduzi ambayo yamevuruga mpito kuelekea utawala wa kiraia na kusababisha wafadhili wa kimataifa kusitisha misaada.

Juhudi za upatanishi zinafanyika kwa siku kadhaa sasa, kutafuta maridhiano kuondokana na mzozo uliopo.

Chanzo cha Habari karibu na Hamdock kilisema Jumatano kwamba hakuna makubaliano yoyote yaliyofikiwa baina yake na viongozi wa kijeshi, na mazungumzo bado yanaendelea.
Utatuzi mgogoro wa Sudan bado haujapatikana Utatuzi mgogoro wa Sudan bado haujapatikana Reviewed by Zero Degree on 11/03/2021 07:45:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.