Loading...

Makambo: Sijachuja, ..Kazi bado inaendelea


Nyota huyo kwa sasa ni kinara wa utupiaji ndani ya Yanga kwenye Kombe la Shirikisho akiwa ametupia mabao matatu, ilikuwa mbele ya Ihefu FC wakati Yanga iliposhinda mabao 4-0.

Mshambuliaji huyo aliweza kuanza pia kwenye mchezo wa jana mbele ya Tanzania Prisons na timu yake ilishinda mabao 2-1 na kusepa na pointi tatu mazima.


Makambo amesema:-“Naona wanasema kwamba uwezo unakuwa umeshuka kwa kuwa sifungi, katika hilo ninasema hapana kwa sababu ili ufunge inabidi uwe unapata nafasi na pia nimekuwa nikifanya mazoezi kila siku jambo ambalo linalinda uwezo wangu.

“Ninachoweza kusema ni kwamba wasubiri, kazi bado inaendelea na kwa namna ambavyo mashabiki wamekuwapamoja nasi kila muda waendelee na moyo huo, sisi tutazidi kupambana kwa ajili ya kupata matokeo,” amesema Makambo
Makambo: Sijachuja, ..Kazi bado inaendelea Makambo: Sijachuja, ..Kazi bado inaendelea Reviewed by Zero Degree on 12/20/2021 12:32:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.