Loading...

Wafungwa watatu wanyongwa nchini Japan



Japan imewanyonga wafungwa watatu leo hii ikiwa ni mara ya kwanza kwa hukumu ya aina hiyo kutekelezwa ndani ya miaka miwili, huku serikali ikisema ni muhimu kuendelea na adhabu ya kifo madhali bado uhalifu wa kikatili unaendelea.

Msemaji wa wizara ya sheria ameliambia shirika la habari la AFP kwamba mmoja kati ya walionyongwa ni Yasutaka Fujishiro mwenye umri wa miaka 65, aliyetumia nyundo na kisu kumuuwa shangaziye wa umri wa miaka 80, binami zake wawili na watu wengine wanne mnamo mwaka 2004.

Wafungwa wengine wawili ni Tomoaki Takanezawa wa umri wa miaka 54, na mshirika wake Mitsunori Onogawa wa umri wa miaka 44 waliowauwa makarani wawili katika jumba la michezo mnamo mwaka 2003.

Japan ni mojawapo ya nchi chache zilizoendelea ambazo bado zinatoa hukumu ya kifo na zenye uungwaji mkono mkubwa wa umma kwa adhabu ya kifo licha ya ukosoaji wa kimataifa.

Chanzo: Dw
Wafungwa watatu wanyongwa nchini Japan Wafungwa watatu wanyongwa nchini Japan Reviewed by Zero Degree on 12/21/2021 10:08:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.