Loading...

Kibu Denis, Dilunga kuikosa Asec Mimosas



MENEJA Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, amefungukia maendeleo ya wachezaji wao Kibu Denis na Hassan Dilunga ambao kwa sasa ni majeruhi.

Hiyo ni katika kuelekea mchezo wa kwanza wa Kombe la Shirikisho Afrika hatua ya makundi dhidi ya Asec Mimosas utakaochezwa Jumapili ya wiki hii kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.

Kwa mujibu wa Spoti Xtra, Ally amesema: “Leo Dilunga ameenda kuangaliwa tatizo lake na kujua niwaniwa muda gani atakaa nje ya uwanja.

“Kwa upande wa Kibu, yeye bado hali yake siyo nzuri, ila Taddeo Lwanga amesharejea na kuanza mazoezi na timu na huenda mwalimu akamtumia katika mchezo  Jumapili.”

Kibu Denis, Dilunga kuikosa Asec Mimosas Kibu Denis, Dilunga kuikosa Asec Mimosas Reviewed by Zero Degree on 2/09/2022 10:11:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.