Loading...

Papa Francis abadilisha idara za mafundisho ya kiimani



Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis, amebadilisha idara za mafundisho ya kiimani, ambazo pamoja na kukuza na kutetea mafundisho ya Kikatoliki pia zitakuwa na jukumu la kushughulikia kesi za unyanyasaji ndani ya Kanisa.

Sehemu ya amri hiyo ya Papa iliyochapishwa leo imesema kufuatia mabadiliko hayo kutakuwa na idara mbili badala ya tatu, ambazo kila moja itakuwa na katibu wake.

Papa Francis aidha ameigawanya mamlaka ya Vatican, upande mmoja ukihusika na mafundisho na upande mwingine utashughulikia nidhamu, na utawala pia umegawanywa kwa kuzingatia idara hizo mbili, badala ya mtu mmoja kama ilivyokuwa awali.

Idara ya nidhamu pia itahusika na kushughulikia masuala ya unyanyasaji, hii ikiwa ni kulingana na Ulrich Rhode, mtaalamu wa sheria ya Kanisa Katoliki, na kuongeza kuwa ni wazi mabadiliko hayo yanaendana na hali ilivyo sasa kufuatia msururu wa madai yaliyoligubika kanisa hilo ya unyanyasaji wa kingono.

Chanzo: Dw
Papa Francis abadilisha idara za mafundisho ya kiimani Papa Francis abadilisha idara za mafundisho ya kiimani Reviewed by Zero Degree on 2/16/2022 11:30:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.