Loading...

Pirates bado inamnyatia Onyango wa Simba SC



VIGOGO wa soka kutoka Afrika Kusini, Orlando Pirates wametajwa kuwa bado kwenye mpango wa kumsajili beki wa kati wa Simba raia wa Kenya, kwa ajili ya Kuimarisha kikosi chao kwa msimu ujao.

Onyango anatarajia kumaliza mkataba wake ndani ya Simba mwishoni mwa msimu huu, ambapo Orlando wanajipanga kutumia nafasi hiyo kumsajili kama mchezaji huru, baada ya dili hilo kushindwa kukamilika kwenye dirisha kubwa la usajili mwaka jana, huku uongozi wa Simba nao ukipambana kumbakisha.

Taarifa kutoka ndani ya Simba zinaeleza kuwa Onyango alikataa ofa ya kusaini mkataba mpya wa kuendelea kusalia ndani ya klabu hiyo, huku akitaka mkataba huo ufanyiwe maboresho ya kimaslahi zaidi kabla ya kuusaini.

“Bado timu ya Orlando Pirates ya Afrika kusini imeonyesha nia ya kumhitaji beki wa Simba, Joash Onyango ambapo baada ya kufahamu kuwa beki huyo anamaliza mkataba mwishoni mwa msimu huu, ambapo wanataka kutumia nafasi hiyo kumsajili bure.” ilieleza taarifa hiyo kutoka Afrika Kusini.

Kwa mujibu wa gazeti la Championi, Ahmed Ally alisema: “Tunajua wapo wachezaji wanaomaliza mikataba yao mwishoni mwa msimu, mpaka sasa hakuna mazungumzo yoyote kutokana na majukumu tuliyonayo kwenye mashindano tunayoshiriki na pia tunasubiri ripoti ya kocha, lakini niwahakikishie Wanasimba kuwa wachezaji wote ambao kocha anawahitaji watapewa mikataba mipya.”
Pirates bado inamnyatia Onyango wa Simba SC Pirates bado inamnyatia Onyango wa Simba SC Reviewed by Zero Degree on 3/31/2022 01:29:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.