Loading...

Ronaldo aomba kuondoka United



MSHAMBULAJI nyota Cristiano Ronaldo ameomba kuruhusiwa kuondoka Manchester United kama itatokea ofa dirisha hili la usajili.

Taarifa zinasema kuwa Mreno huyo mwenye umri wa miaka 37 sasa anataka kucheza Ligi ya Mabingwa tena msimu ujao.

Ronaldo ndiye mfungaji Bora wa Man United msimu uliomalizika, akiwa na jumla ya mabao 24, lakini Mashetani hao Wekundu walimaliza Ligi Kuu ya England katika nafasi ya sita.

Ronaldo alirejea Old Trafford msimu uliopita akitokea Juventus na amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake wa sasa klabuni hapo.

Na inafahamika kuwa Chelsea, Bayern Munich na Napoli ni miongoni mwa klabu kubwa ambazo tayari zimeonyesha nia ya kumsajili nguli huyo wa kupachika mabao.
Ronaldo aomba kuondoka United Ronaldo aomba kuondoka United Reviewed by Zero Degree on 7/08/2022 09:22:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.