Loading...

Chelsea yaishangaza United ndani ya dakika za lala salama


Cole Palmer alifunga mabao mawili ndani ya dakika za lala salama na kukamilisha hat-trick yake na kuipatia Chelsea ushindi wa ajabu dhidi ya Manchester United licha ya hapo awali kuwacha uongoza wa mabao mawili.

Hatua hiyo inajiri huku Liverpool wakiwashinda wageni wao Sheffield United 3-1 na kupanda hadi kilele cha ligi kuu ya England.

Bao la ushindi la hivi punde zaidi lililofungwa katika historia ya Premier League, katika dakika 100 na sekunde 39, liliwashangaza United, ambao walitangulia dakika tisa za majeruhi, na kupelekea Stamford Bridge kutapatapa.

United walikuwa mbele kwa dakika 99 na sekunde 17, ikiwa timu ambayo imewahi kuongoza katika mechi ya Ligi Kuu ya Uingereza na kushindwa.

Mapigo hayo mawili ya dakika za lala salama yalimalizia mchezo ambao ulianza kwa kasi, huku nahodha wa The Blues, Conor Gallagher akiwaweka mbele wenyeji.

Ndani ya dakika 20 Palmer alifunga bao la pili la wenyeji baada ya Antony kumchezea vibaya Marc Cucurella.

Lakini Alejandro Garnacho aliamsha matumaini ya ushindi wa United alipoingilia kati pasi ya Moises Caicedo kwenye eneo la nyuma.

Bruno Fernandes aliisawazishia United dakika tano baadaye alipounganisha kwa kichwa krosi ya Diogo Dalot.

Bao la pili lilifungwa na Garnacho akiunganisha kwa kichwa mpira uliopigwa kutoka kwa Antony na kumpita kipa Djordje Petrovic, na kuwapa United matumaini ya ushindi, matumaini yaliyozimwa na 
Cole Palmer aliyefunga mabao mawili ndani ya dakika za lala salama.

Mechi hiyo ilimalizika kwa kishindo huku Chelsea ikitwaa pointi zote tatu.
Chelsea yaishangaza United ndani ya dakika za lala salama Chelsea yaishangaza United ndani ya dakika za lala salama Reviewed by Zero Degree on 4/05/2024 06:35:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.