Dkt. Biteko awasili Pemba kwa ajili ya maandalizi ya maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewasili Kisiwani Pemba na kupokelewa na Waziri ofisi ya Makamo wa Rais, Sera, Uratibu na Baraza la wawakilishi Mhe. Hamza Hassan Juma kwa ajili ya shughuli za maandalizi ya maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yatakayofikia kilele chake terehe 26 April 2024.
Akiwa Kisiwani humo Dkt. Biteko ataweka jiwe la Msingi wa Ujenzi wa kituo cha Afya, Shehia ya kinyikani Jimbo la Kojani Wilaya ya Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba.
📍Pemba - Zanzibar.
Dkt. Biteko awasili Pemba kwa ajili ya maandalizi ya maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano
Reviewed by Zero Degree
on
4/20/2024 01:40:00 PM
Rating:
