Loading...

Lori laua wawili mkoani Njombe


Watu wawili akiwemo Dereva wa Lori wamefariki dunia baada ya gari hilo kupinduka katika eneo la Lihogosa lililopo Halmashauri ya wilaya ya Wanging’ombe mkoani Njombe.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Mahamoid Banga alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo April 19, 2024.

Kamanda Banga alisema chanzo cha ajali hiyo ni lori lilikwaruzana na Lori lingine la makaa ya mawe likiwa linatokea Makambako kuelekea Songea na kisha Kupinduka.

“Dereva wa Lori la mbao alipoteza maisha papo hapo pamoja na mmiliki wa mzigo wa mbao lakini utingo wa lori ni majeruhi na amelazwa Hospitali ya Rufaa ya Njombe, amesema Banga.


“Mpaka sasa dereva wa lori la makaa ya mawe hajakamatwa ili ahojiwe kuhusu ajali hiyo,” ameongeza Kamanda Banga.

Waliofariki dunia ni Dereva wa lori hilo Bryson Kihombo (30) na Juma Joseph (43), mmiliki wa mzigo wa mbao ambazo zilikuwa zikisafirishwa kuelekea Jijini Dar es Salaam.

Cc: Tanzaniaweb.Live
Lori laua wawili mkoani Njombe Lori laua wawili mkoani Njombe Reviewed by Zero Degree on 4/20/2024 06:16:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.