Loading...

Makalla Katibu mpya wa Itikadi na Uenezi CCM



Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi, imekutana hii leo chini ya Mwenyekiti wake na Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

Imefanya mabadiliko madogo ya Sekreterieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ambapo Amos Makalla amechaguliwa kuwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi na Uenezi na Mafunzo, akichukua nafasi ya Paul Makonda ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha.

John Mongella amechaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa CCM Bara, akichukua nafasi ya Anamringi Macha ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.

Wajumbe wengine ni pamoja na Jokate Mwegelo amechaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM, ambaye hapo kabla alikuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake wa chama hicho.

Kadhalika Ally Salum Hapi amekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Wazazi Tanzania.
Makalla Katibu mpya wa Itikadi na Uenezi CCM Makalla Katibu mpya wa Itikadi na Uenezi CCM Reviewed by Zero Degree on 4/03/2024 06:36:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.